Msanii wa Bongo move, Devota Mbaga
hivi karibuni alipatwa na kisanga cha mwaka baada ya kuvuliwa nguo na
maofisa wa uhamiaji alipoenda Hong Kong, nchini China kwa ajili ya
shughuli zake za kibiashara.
Kwa mujibu wa staa huyo, alifanyiwa
kitendo hicho cha kuvuliwa nguo zote na maofisa wa uhamiaji mara
alipotua Uwanja wa Ndege wa Hong Kong na kumsachi kwa kuhofiwa kuwa
amebeba ‘unga’.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa
njia ya simu, Devota alisema baada ya kuvuliwa, alishikwa sehemu zake za
siri kitendo alichokiita ni cha kidhalilishaji.
“Ilikuwa ni baada ya kugongewa
pasipoti yangu nikaingizwa kwenye kitengo cha polisi wa madawa ya
kulevya ambao walinitaka nivue nguo zote ili nikaguliwe,” alisema kwa
masikitiko.
Msanii huyo alisema mbaya zaidi siku hiyo alikuwa katika mzunguko wake wa mwezi lakini maofisa hao hawakujali.
Kama vile haitoshi, Devota alisema
kuwa, baada ya kumalizika kwa zoezi hilo maofisa hao walimchezea sehemu
za kifuani huku wakimwambia kama hakutaka kufanyiwa hivyo angerudishwa
alikotoka.
“Kwa kweli nimeumia sana kwa kitendo
nilichofanyiwa, nimeshinda nikilia kutwa nzima na kila nikikumbuka
naumia,” alisema Devota.
No comments:
Post a Comment