TTCL

EQUITY

Monday, October 14, 2013

TUMUENZI HAYATI BABA WA TAIFA KWA VITENDO

LEO NI NYERERE DAY HEBU ANGALIA NA FAHAMU MACHACHE TOKA KATIKA MAKUMBUSHO YA MWALIMU JULIUS. K.NYERERE

Hili ni jumba la Makumbusho ya Mwalimu J.K.Nyerere, Butiama mkoani Mara. Ushawahi kutembelea hapa?


Mchezo wa Bao huchezwa na makabila mengi hapanchini Mwalimu J.K Nyerere amekuwa akicheza na kuupenda mchezo huo hata baadhi ya vyama miaka ya sasa kumuenzi kwa kufanya mashindano mbalimbali nchini. Bao hili alipewa na wananchi wa Ndanda.

Joho la Uhitimu.

Hivi ni baadhi ya viatu alivyokuwa akivaa Hayati Mwalimu J.K.Nyerere. Mwalimu alipenda zaidi viatu vya kutumbukiza, pembeni kama mkoba ni redio yake. Itizame kwa uzuri katika picha inayofuata.

 


Ni Redio aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kusikiliza habari mbalimbali alipenda pia kuitumia katika baadhi ya ziara zake za ndani na nje ya nchi. Redio hii alipewa zawadi huko Ujerumani mwaka 1969.

A gift of traditional stool given to Mwl. Nyerere by the residents of Dar-es-Salaam after the victory of Kagera war in 1978 - 1979.

Jiwe la kusagia nafaka huitwa 'Ombwe' na dogo huitwa Esyo, kwa kawaida kazi ya kusaga hufanywa na wanawake. Chakula kikuu cha wazanaki ni ugali, huliwa kwa nyama, samaki na mboga za majani.

Picha nazo zipo

Urithi wa asili wa Tamaduni za kizanaki silaha za jadi, vifaa vya nyumbani, ala za muziki, mapambo ya asili, lugha, mila, desturi - nk. Vyte utavikuta kwenye nyumba hii ya makumbusho ya Mwalimu.

No comments:

Post a Comment