DR. SLAA; SASA NIMEMALIZA ZIARA....
Katibu
Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amemaliza ziara ya wiki tatu nchini
Marekani aliyoalikwa na Umoja wa vyuo vikuu vikubwa nchini humo.
Ziara hiyo iliyomchukua kiongozi huyo majimbo mbalimbali ilipewa jina
la 'Vision Tanzania' na ilikuwa ya manufaa makubwa kwake,kwa chama chake
na kwa Taifa lake.
Akizungumza jana Jumapili akiwa uwanja wa
ndege Marekani kabla ya kuondoka Dr Slaa alisema amejifunza mambo mengi
sana ambayo ni faida kubwa kwa Watanzania.
Dr Slaa amekuwa gumzo Marekani katika majimbo kadhaa aliyotembelea
kutokana na hotuba alizokuwa anatoa katika vyuo vikuu na sehemu
nyinginezo alizotembelea ikiwemo shirika la Anga.
Katika hotuba
iliyotikisa wazungu ni pale kiongozi huyo nyota wa Tanzania aliposema
CHADEMA haitaki pesa za wamarekani bali wanachokitaka kutoka kwao ni
Utaalamu wao (Skills).Hotuba ya Dr Slaa na uthubutu wake mbele ya
wazungu imesababishwa kufananishwa na Hotuba za Mwl Nyerere aliyekuwa
anawakemea wazungu bila woga.
Wiki hii mitandao ya kijamii
nchini Kenya ilitawaliwa na Hotuba ya Dr Slaa iliyosambazwa na
kuchukuliwa kama 'The greatest speech from African Politician'
Dr Slaa anawasili nchini huku Muungano wa Upinzani ukitarajiwa kukutana na Rais Kikwete kesho kujadili mustakabali wa Katiba.
No comments:
Post a Comment