Mkurugenzi "Tunaieshimu Arusha kwa heshima iliyonayo ndani na nje ya Tanzania, hivyo tunaahidi kufanya mazuri na yenyekuleta heshima kwa Nchi yetu na Watanzania"
Watatu kutoka kulia ni Mwenye kiti wa Swahili arts group Bw. Amani John Masuka akiwa na viongozi wa swahili pamoja na Meneja wa Barafu kwenye kikao |
Mkurugenzi mkuu wa Swahili arts group Bw. Aman John Masuka hileo
amekamilisha kikao cha uratibu na uendeshaji wa shughuli za club hiyo kikao
ambacho kimechukua siku mbili huku kikihitaji umakini mkubwa, Kikao ambacho kilikuwa
sio rasmi aliitisha mkurugenzi ambapo kiliwahusisha viongozi wote wa kundi la Swahili,
na hatimaye leo kimefikia tamati baada ya kuiweka mikakati yote katika kusudi
lililo pangwa na kuaziimia kwa pamoja kuhakikisha wanakwenda kuiweka Swahili arts
group katika taswira njema, na kuijengea heshima kwa jamii, mashabiki, wageni
ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Katika kikao hicho kilicho wa kutanisha viongozi wote wa Swahili
arts group mada kuu ilikuwa ni ripoti ya maandalizi ya shoo itarajiwayo
kufanyika ijumaa tarehe 18/10/2013 katika viwanja vya BARAFU zamani vikijulikana kama MASAI CUMP, PIA ILIFUATIWA Project ya
mafunzo ya ukimwi kwa vijana wenye umri miaka (15-28), Bw. Seif Mziray ambaye
ni meneja wa Swahili alishauri kuwepo
kwa kikao kitakachowakutanisha waalimu wa shule za msingi na sekondari kama
wahusika wakuu ambapo watachambuliwa azma ya kuwepo kwa project hiyo ya Swahili
na lengo kusudiwa la kukutana na watoto hao.
Mkurugenzi pia alihusisha swala la ukamilishaji wa filamu ambayo
hivi sasa zikiwa zimebaki sehemu 10 ili kukamilika na baadhi yake zikiwa
zimekamilika, ambapo alieleza hadi sasa amekwisha gharimika kiasi cha zaidi ya
laki tano kutokana na baadhi ya mahitaji muhimu yaliyolazimu fedha ikiwemo kukodi
kamera, usafiri, gharama za usajili na kuendelea kusema gharama hizo zote
ziliugharimu mfuko wake yeye binafsi na hivyo pahala walipo fika binafsi
anamshukuru Mungu. Mkurugenzi akisema kwa furaha na mwenye tabasamu alisema
kuwa vipande vilivyo baki havina gharama kubwa napia hatua iliyobaki ni ndogo
tofauti walipoanza.
Aidha mada nyingine iliyo zungumziwa ilikuwa uzinduzi na
arambee ya mfuko wa Swahili, Swahili ikiwa kama taasisi ya sanaa yenye lengo la
kuibua vipaji na kutengeneza soko la ajira ya kudumu kwa vijana walio wengi
wenye Elimu ya juu na vipaji jiji Arusha Swahili imedhamiria kuwa mkombozi wao,
kwa kujipanga na uzinduzi utakaoenda sambamba na utambulisho wa filamu yao iliyo
beba ujumbe muhimu kwa jamii, ambapo itakuwa surprise kwa wageni na mashabiki
wao. Vilevile mkurugenzi alifafanua leongo la uzinduzi na kusema kuwa ni kutoa
utambulisho wa Swahili arts group, kuionesha jamii kilekinachofanywa na Swahili
ikiwa ni kukemea maovu kama vile ukatili wa kijinsia, biashara na matumizi ya
madawa ya kulevya, kufundisha kuhusu ukimwi, tatizo la ajira na kuwa mfano bora
wa kuigwa na jamii kwa kutofanya maovu na kushirikiana nayo. kwa maoni na ushauri tembelea ukurasa wetu hapa Swahili Arts Group
No comments:
Post a Comment