TTCL

EQUITY

Sunday, September 29, 2013

GUMZO LA JIJI; RAY C AMZIMIKIA "ABDUL HAJI" SHUJAA WA WESTGATE ALIYE OKOA WATU WENGI KUTOKA MIKONONI MWA MAGAIDI

Abdul Haji ni miongoni mwa mashujaa ambao hawatasahaulika nchini Kenya kutokana na kuamua kuhatarisha maisha yao ili kuokoa watu waliokuwa wamekwama ndani ya jengo la Westagate baada ya kushambuliwa na Al-Shabaab Jumamosi iliyopita.


Tangu asimulie namna alivyopambana na magaidi hao, Haji ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi hasa wasichana na mmoja wa watu aliowagusa ni Rehema Chalamila ambaye amesema anatamani mwanaume mjasiri kama yeye ambaye watazaa naye watoto.

“In love with ths Soldier!i want a soldier like him to marry me,” ameandika Ray C kwenye picha ya gazeti aliyoipost kwenye Instagram ikimuonesha Abdul Haji.

“I love You Abdul Haji,You are my Heroooooooo,” aliandika Ray C kwenye picha nyingine.

Kwenye picha nyingine Ray C aliongeza, “My soldier,My Prince,My Love….Love You Abdul Haji.”

Kijana huyo ni mtoto wa waziri wa zamani wa ulinzi nchini Kenya ambaye alienda kwenye mall hiyo baada ya kupata ujumbe kutoka kwa rafiki yake kuwa kaka yake alikuwa ndani ya Westgate wakati watu hao wenye silaha walipovamia.

Akiongea na NTV, Haji ambaye sio mwanajeshi, alisema alifundishwa kutumia bunduki na baba yake ili kulinda mifugo yao isiibiwe na wezi.

Ujuzi huo ulimsaidia Jumamosi hiyo kuwasaidia wafanyakazi wa Red Cross wafanye kazi yao kwa usalama kwa saa tatu na kusaidia kuokolewa kwa watu wafikao 1,000 nje ya mall hiyo.

No comments:

Post a Comment