TTCL

EQUITY

Sunday, September 29, 2013

HII NDIO TAFSIRI YA KISWAILI YA MAHOJIANO YA MSEMAJI WA AL-SHABAAB JUU YA UVAMIZI NA MAUAJI YA WATU KENYA


Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?

Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda. Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.

JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?

Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya. Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si wadhaifu. Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.

JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?

Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo. Sababu tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya jiji. Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile Mkenya.

JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?

Msemaji:
 Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.

JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?

Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.

JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?

Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.

JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?

Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.

JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?

Msemaji:
 Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.

JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?

Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.

JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?

Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia. Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya.

No comments:

Post a Comment