
Rais
Jakaya Kikwete ametembelea raia wawili wa uingereza waliolazwa katika
hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es salaam baada ya Kumwagiwa tindikali
na watu wasiojulikana huko visiwani Zanzibar.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam
baada ya kuwatembelea raia hao wawili ambao ni Katie Gee na mwenzake
Krist Trup wenye umri wa miaka 18 kila mmoja,rais Kikwete amesema
ameskitishwa na tukio hilo na kwamba wakati wanaendelea kupewa matibabu
vyombo vya usalama vinaendelea kufanya kazi yake ili kubaini waliohusika
na tukio hilo ambalo Mh rais amesema ni tukio la aibu
Mwenyeji wa wagonjwa hao waliomwagiwa na tindikali na watu
wasiojulikana,Bwana Bashir Ismael kutoka visiwani zanzibar,amesema raia
hao walilkuja hapo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kufundisha na kwamba
ni walimu wa shule ya St Monica inayomilikiwa na moja ya taasisi za dini
ya kikiristo ambalo lipo eneo la mkunazini stone town.
Baada ya mh rais kuwatembelea wagonjwa hao,alipita katika chumba
kingine kumjulia hali mbunge wa jimbo la bariadi Mh John Momose Cheyo
aliyelazwa katika hospitali hiyo ya Aga Khan kutokana na tatizo la
shinikizo la damu ambapo kwa mujibu wa mpwa wa mbunge huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Bwana Wanjoda Mwinamila,amesema Mh Cheyo
anaendelea vizuri
No comments:
Post a Comment