TTCL

EQUITY

Saturday, August 24, 2013

Mchuuzi wa maziwa apewa kichapo kwa kumchafua ng’ombe

Embu Mji wa Embu. Picha/MAKTABA

MCHUUZI wa maziwa mwenye umri wa miaka 50 alipata majeraha mabaya, aliposhambuliwa na umma kwa kupatikana akifanya mapenzi na ng’ombe katika kijiji cha Kabogi eneo la Kathaari, Embu Kaskazini.
Bw Nyaga Kirianye anadaiwa kufumaniwa na mkulima mmoja katika eneo hilo akimchafua ng’ombe huyo mwendo wa saa tatu na nusu asubuhi.
Mkulima huyo alipiga kamsa iliyowavutia wanakijiji ambao walimpa kichapo cha mbwa kabla ya kuokolewa na naibu wa chifu wa eneo hilo.
Wenyeji walidai ya kuwa mfanyabiashara huyo ana mazoea ya kuwafukuza wake zake na inadaiwa alimfukuza mke wake wa hivi karibuni, miezi miwili iliyopita.
Bw Kirianye alijitetea kwa majirani akisema yeye huwa anavutiwa na ng’ombe huyo kwa vile hana mke.
Alipelekwa katika kambi ya chifu akingojea kufikishwa hospitalini kabla ya kufunguliwa mashtaka.

No comments:

Post a Comment