Bw Francis Kimemia (kushoto) akiwa kortin
OMBI la katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Kimemia kutaka
atoe ushahidi faraghani dhidi ya mwanablogu aliyedai mtumishi huyo mkuu
wa umma alifanya mkutano wa siri Alhamisi lilikataliwa na mahakama.
Bw Kimemia alilazimika kutoa
ushahidi wake mahakamani baada ya mshtakiwa Robert Alai kupinga ombi
hilo la kufanyiwa kesi faraghani akisema “hakuna sheria inayoruhusu hayo
akiongeza afisa huyo mkuu wa serikali sio maalum ili akubaliwe kutoa
ushahidi kwa siri.”
Hakimu mwandamizi Joseph Karanja wa
Mahakama ya Milimani Nairobi alikataa ombi hilo la Bw Kimemia,
mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) Isaac Hassan
Bw Kimemia aliamriwa afike kortini
kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Bw Alai ya kuchapisha habari
katika mtandao kwamba katibu huyo alikuwa anakutana na Jaji Isaac
Lenaola, mwenyekiti wa IEBC Ahmed Isaack Hassan na aliyekuwa wakati
mmoja mkuu wa polisi Meja Jenerali Mstaafu Mohammed Hussein Ali.
Bw Kimemia alidaiwa alikuwa
anajaribu kuwashawishi kuhusu kesi ya kupinga uchaguzi wa Rais Uhuru
Kenyatta na Bw Raila Odinga iliyokuwa inasikizwa katika Mahakama ya Juu.
“Sijawahi kutana na watu hao wanaodaiwa nilikutana nao na kamwe sijawahi kukutana na Alai,” alisema Bw Kimemia.
Bw Alai ameshtakiwa kwa kutuma ujumbe wa kuudhi.
Alhamisi wakili anayemtetea Bw Alai
alimtaka Bw Kimemia awasilishe thibitisho kwamba ni yeye alichapisha
ujumbe huo katika mtandao.
Katibu huyo alisema maafisa wanaochunguza kesi hiyo wanajua jinsi walimuhusisha Bw Alai na taarifa hizo.
“Nilifahamishwa na marafiki kwamba
kulikuwa na taarifa katika mtandao kwamba nilikutana na Jaji Lenaola,
mwenyekiti wa IEBC Bw Ahmed Isaack Hassan na aliyekuwa Kamishna wa
Polisi Meja generali (mstaafu) Ali Mohammed,” alisema Bw Kimemia.
Kuapishwa
Alisema wakati taarifa hizo zilikuwa
zinachapishwa alikuwa mwenyekiti wa kamati andalizi ya sherehe za
kuapishwa kwa rais mpya na kwamba watu wengi walikuwa wanasoma taarifa
alizotuma Alai.
“Hakukuwa na ukweli wowote kwamba
nilikuwa nakutana na watu hao katika kilabu cha Karen Blixen,” Bw
Kimemia alimweleza Bw Karanja na kuongeza "sijui nilikuwa wapi siku
niliyofahamishwa kuhusu ujumbe huo uliotumwa katika mtandao.”
Alisema hakuwapigia watumishi wenzake simu kwa vile “taarifa hizo zilikuwa za uwongo.”
“Kama afisa mkuu wa serikali taarifa
hizo zilinikera na kuniahibisha mbali na kudai kwamba sifai kuhudumu
katika wadhifa wangu,” alisema.
Alisema alimpigia simu Mkurugenzi wa CID Ndegwa Muhoro achunguze taarifa hizo.
Bw Kimemia alisema punde tu kesi hiyo itakapokamilika atamshtaki Bw Alai kwa kumharibia jina.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 6.
No comments:
Post a Comment