Unajua ilikuwaje?
Dogo kaja anataka kujua kama andagraundi
wataruhusiwa kupafomu ama nini? Mimi siyo sekta yangu nikamwambia mstue
dazeni ndiyo ishu zake hizo mimi mtu wa `nyuzpepaz’.
Kanigomea kudadadeki zake, haukamz? Mi wewe ndiyo nakujua kwa hiyo kama vipi we nenda kamstue, mi nakungoja hapa unipe jibu.
Nikamuuliza kwa hiyo dogo unanituma?
Dogo unafikiri kajibu? Akanikunjia uso akawa
ananicheki tu. Sasa mi si unanijua mtu mzima? Nikashtukia tu kwamba hizi
ni `rizati’ za ganja za utotoni, unajua ganja nazo bwana ukizianza
mapema unaweza ukamzingua hata dingi yako, mi nikajifanya kama naenda
kumshtua dazen, nikaishia huko huko sikurudi.
Enewei tulikuwa Tabora kwenye Fiesta na leo
nimelikita ukweni unaambiwa. Kila demu ninayemsalimia ananiita shemeji,
najiuliza haukamz kudadadeki?
Eneweiz mashemeji mziki upo kesho, karibuni uwanjani chama kubwa Mwanaspoti linakuja kukamua ndani ya Fiesta, mnanisoma?
sasa leo nataka tudiskasi mambo ya adabu kidogo
sababu mwanangu mwenyewe Kandoro yamemkuta rodini huko kwenye mitikasi
yake, na haya mambo ya mjini ...kikanuka ile ile kudadadeki.
Uliza ilikuwaje?
Mwana alikuwa anakula ndefu, mitaa ya baga nini
akaskilizie upepo wa baharini, si unajua zile? Basi mwanangu katika
kukamua nini barabarani si likaibuka daladala, likawa kama linataka
kumchomekea, akaona ujinga, akamkazia. Kumkazia na mwenye daladala naye
akawa kama anakaza hivi, kha ...kikalia mwanangu kizinga.
Halafu mwanangu alikuwa anasukuma kitu cha
mjerumani, kikawa kama kimeparuzwa upande mzima hivi, ikabidi, Kandoro
ashuke, akaenda kuchomoa funguo za daladala, akaenda mbele ya gari lake,
akawa kalikita anasubiri mwafaka wa nini kije kufuata baada ya ajali.
Uliza nini sasa?
Alishuka mshua huyo kaenda eji kuliko matarajio
unaambiwa, fulu mvi kichwani unaambiwa akamuendea Kandoro, akaanza
kumletea za kiutu uzima zile za “...hujambo mwanangu?”.
Kandoro nguvu kama zikamwishia hivi unaambiwa,
kabla hajamjibu unaambiwa dingi akajitupa chini akaanza kumshika miguu
Kandoro, anamwomba msamaha, hadithi kibao unaambiwa zikaanza
kum’mwagika.
Unaambiwa mzee akaanza kuleta zile za
“...mwanangu, unajua siyo mimi, wadogo zako nyumbani ndiyo wanayataka
haya, kama wangesoma mimi saa hizi ningekuwa nimepumzika, lakini inabidi
babaako nihangaike na dunia, nakuomba radhi mwanangu nisamehe niko
chini ya miguu yako”.
Mshua alipoona Kandoro haoneshi kujali akaanza
kuangusha na chozi yaishe, unaambiwa kalia kama mtoto mdogo mpaka kila
mtu akawa anamwonea huruma.
Ilibidi Kandoro amteme yule dingi aende zake
lakini ndiyo akawa kashakula losi ya maana kutokana na mazingulizi ya
mshua. Mi nilikuwa pembeni hapo nashuhudia muvi zima nikajiuliza ina
maana huyu mshua alipokuwa anakaza alikuwa hakumbuki kama kuna watoto
homu?
Au ndiyo kwa sababu alikuwa anasukuma daladala, akawekeza na akili zake kidaladala?
Mimi kama zee nawaambia washua wote ambao wana
hizi ishu za kujitoa akili wanapokuwa katika mitikasi ya town kwamba
siku wakiingia katika kumi na mbili zangu...
Tutaelewana hakyanani.
Singida, kesho basi uwanjani pale tukaone itakuwaje au siyo?
Pamoja!
No comments:
Post a Comment