Charles Darwin kijana
Charles Robert Darwin
(12 Februari
1809 - 19 Aprili 1882) alikuwa
mwanasayansi Mwingereza
katika karne ya 19.
Nadharia hii yasema kuwa spishi zote za
viumbehai vimetokana na spishi asilia zilizogeuka baada ya muda. Mageuko haya
hufuata uteuzi
asilia yaani viumbehai wanaolingana vizuri zaidi na
mazingira wanaishi na kuzaa kushinda viumbehai wasiolingana nayo.
Kwa njia hiyo tabia za viumbehai wanaofaa vizuri zaidi
zinazidi kuendelezwa kwa sababu watoto wao hurithi tabia hizi. Lakini tabia za
viumbehai wasiofaa sana zinaweza kutoweka kwa sababu wanakufa mapema na hawana
watoto wengi wanaoendeleza tabia zao.
Utoto na masomo
Alizaliwa mjini Shrewsbury (Uingereza)
kama mtoto wa tano wa daktari Robert Darwin na Susannah Darwin (née Wedgwood).
Baada ya kumaliza shule alijiunga na chuo kikuu cha Edinburgh (Uskoti) 1825
akajiandikisha katika idara ya tiba lakini
hakupenda upasuaji. Alitumia muda mwingi kufuata kozi za biolojia, jiografia na jiolojia nje ya masomo
ya tiba. Alifuatana mara nyingi na wataalamu walipofanya uchunguzi wa wanyama,
mimea au mawe.
Baba baada ya kuona hafai kuwa daktari alimwandikisha
katika masomo ya dini kwa shabaha ya kuwa mchungaji wa kanisa la kianglikana
aliyomaliza mwaka 1831.
Safari ya MS Beagle
Safari ya Darwin kwenye Beagle
Baada ya kumaliza masomo haya Darwin alipata nafasi ya
kujiunga kama mshiriki na safari ya kisayansi ya jahazi MS
Beagle iliyotakiwa kuzunguka dunia yote kwa kusudi la
kuboresha ramani hasa za pwani la Amerika Kusini. Darwin alipewa nafasi ya mwanaviumbe bila malipo ya
kuongozana na kushauriana na nahodha na kiongozi wa safari kuhusu wanyama na mimea
visivyojulikana na vitakavyopatikana safarini.
Katika safari hii Darwin aliona Amerika Kusini na visiwa vya Pasifiki. Akaona mengi
na kushika kumbukumbu yake akakusanya mimea na miili ya wanyama na kuibeba naye
kwa ajili ya maonyesho katika jumba la makumbusha la historia ya viumbe.
Kwenye visiwa vya Galapagos aliona ya
kwamba kila kisiwa kilikuwa na spishi za ndege pia
kobe zilivyotofautiana kidogo kati ya kisiwa na kisiwa.
Nakala ya 1859 ya kitabu Origins of
Species
Mapinduzi ya kisayansi
Baada ya kurudi Uingereza mwaka 1836 Darwin alianza
kuchunguza sampuli zote alizokusanya. Alipata kazi kama katibu wa shirika la
jiolojia.
Alipochungulia sampuli za Galapagos hasa alipata
dhana ya kwamba spishi hizi zote za karibu zilitokana na aina moja tu iliyowahi
kufika kwenye visiwa hivyo lakini baadaye zilianza kuwa tofauti katika kila
kisiwa na kuwa spishi ya pekee. Kama hiyo ilikuwa kweli spishi hizi hazikuumbwa
hivyo tangu mwanzo.
Darwin aliendelea na utafiti wa sampuli zake na kutoa
masomo mbalimbali na kuyatafakari. 1859 alitoa kitabu
kuhusu mageuko ya
spishi kwa njia ya uteuzi
asilia (On the Origin of Species by Means
of Natural Selection, or the Preservation of Favoured Races in the Struggle for
Life) alimoeleza nadharia yake.
Kitabu kilikuwa kama bomu kati ya watu wa sayansi na
wa dini.
Darwin alishambuliwa mara nyingi ya kuwa mafundisho
yake yanapinga taarifa ya uumbaji
katika Biblia.
Lakini hiyo inategemea jinsi masimulizi yake yanavyosomwa: si lazima mwamini
achukue kila kitu kama ilivyoandikwa, kwa sababu Biblia hailengi kutufundisha
sayansi, bali njia ya wokovu.
Leo hii nadharia yake inakubaliwa na wanasayansi
karibu wote hata kama bado kuna kiasi cha upingamizi dhidi yake kwa sababu za
kisayansi na za kidini..
No comments:
Post a Comment