Ilidaiwa kabla ya hapo, wakati
wakicheza, kulitokea ugomvi kati yake na mwenzake aliyekuwa akicheza
naye, Nyanswi Magaigwa, baada ya Joseph kuliwa Sh 5,000.
Katika ugomvi huo, inadaiwa Magaigwa
alichukua panga na kumjeruhi mwenzake shingoni na kisogoni, ambapo
majeruhi alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya na kupatiwa matibabu
kabla ya kurejeshwa nyumbani.
Kamanda Kamugisha alisema Joseph
aliendelea kupatiwa matibabu akitoka nyumbani na ilipofika Agosti 4 saa
moja asubuhi, alifariki dunia na mwili wake ulipofanyiwa uchunguzi,
ilibainika chanzo cha kifo chake ni jeraha alilopata shingoni.
Polisi inamsaka mtuhumiwa na raia wema
wameombwa kutoa taarifa mara watakapomwona Nyanswi, ili aweze kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
Wakati huo huo katika kijiji cha Kinesi,
kata ya Nyamunga, wilayani Rorya, mtoto Baraka Chacha (4), amechoma
nyumba wakati akichezea kiberiti.
Baraka ambaye hakupata majeraha baada ya
kuokolewa, alipokuwa akichezea kiberiti, inadaiwa aliwasha moto godoro
na kusababisha usambae katika nyumba nzima, mali ya William Mabala.
Kamanda Kamugisha amewatahadhalisha
Wazazi kuwazuia Watoto wao kuchezea moto kwani hasara kama hiyo
imesababishwa na wazazi kutowakanya watoto wao kuchezea moto.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/afariki-baada-ya-kujeruhiwa-na-panga.html#ixzz2bSOWVyj6
No comments:
Post a Comment