Tumuombee apone mapema
Nelson Mandela amekaa kwa siku ya pili hospitalini akiwa mahututi, huku
hofu ikizidi kuwa shujaa huyo wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi
wa rangu huenda akapoteza mapambano yake ya mwisho.
Licha ya jitihada za kila aina kutoka kwa madaktari katika hospitali ya
Mediclinic ya mjini Pretoria, hali ya mpambanaji huyo mwenye umri wa
miaka 94 imeendelea kudorora katika siku za hivi karibuni. Raia wa
Afrika Kusini wamekuwa wanapita karibu na nyumba ya Mandela mjini
Johannesburg na kusema wanamuombea, baada ya rais Jacob Zuma kutoa wito
kwa taifa hilo kumuombea Mandela ambae alimuita baba wa demokrasia.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel alipomtembelea Mandela mjini Johannesburg, 6.10.2007
Siku ya Jumatatu, rais Zuma aliuambia umma uliokuwa na shauku kubwa
katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia Televisheni, kuwa
Mandela anaendela kuwa katika hali mbaya sana hospitalini, na kuongeza
kuwa madaktari walikuwa wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha ustawi
wake. Mke wake wa zamani Winnie Mandela, ambae pia alitoa mchango mkubwa
katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, mabinti zake Zindzi
Mandela-Motlhajwa na Zenani Mandela-Dlamini, na maafisa kadhaa wa
serikali walikwenda hosptiali jana Jumatatu kumjulia hali.Hofu yazidi kutanda
Ziara hizi za jamaa zake Mandela, licha ya kuwa za kawaida tangu alipolazwa siku 18 zilizopita, zinakuja huku kukiwa na hofu zaidi kuhusu hali ya afya yake. Binti yake mkubwa Makaziwe amesema baba yake yuko katika amani na nafsi yake, huku akilalamika juu ya kile alichokiita wazimu wa vyomba vya habari kuhusu hali ya baba yake. Gazeti la Sowetan la mjini Johannesburg, limeripoti leo kuwa wanafamilia wameitisha kikao cha dharura kijijini kwao kujadili matatizo ya kiafya ya Mandela.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Ujumbe wa kumtakia ahueni Mandela umetoka pia ng'ambo. Mjini Washington, ikulu ya Marekani ilisema inamuombea Mandela. Rais wa Marekani Barack Obama kesho Jumatano anaanza ziara yake ya bara la Afrika, itakayomfikisha nchini Afrika Kusini, Senegal na Tanzania. White House ilisema inafuatilia hali ya afya ya Mandela, na haijasema iwapo kuzidi kudorora kwa afya hiyo kutaathiri ziara hiyo. Mandela atatimiza miaka 95 ya kuzaliwa Julai 18.
No comments:
Post a Comment