TTCL

EQUITY

Thursday, June 27, 2013

NIDHAMU KUZINGATIWA

Wazuiwa Chuo Kwa Nguo Waliyovaa

NewsImages/6885854.jpg
wanafunzi waliyofukuzwa

Katika hali ya kupambana na kasi ya mmomonyoko wa maadili nchini Jordan, Wanafunzi watatu wa kike wazuiwa kuingia darasani kwa sababu ya ugeni wa nguo walizovaa, kwa madai kuwa kinyume na maadili ya chuo hicho.
Wakati baadhi ya wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu nchini Tanzania, wakilalamikiwa kuwa nguo ambazo wanazovaa ni kinyume na maadili ya kitanzania na zinachochea kwa kiasi kikubwa vitendo vya ngono zembe.

Hali ni tufauti huko nchini Jordan, Chuo Kikuu cha Petra Jodan, kimefikia uwamuzi wa kuwazuia wanafunzi wake watatu wa kike nje ya jengo la chuo hicho katika lango kuu la kungilia chuoni hapo kwa sababu ya mavazi waliyovaa wanafunzi hao.

Kutokana na ugeni wa vazi walilolivaa wanafunzi hao chuoni hapo, walipewa jina la wasichana wa baraka, wanafunzi hao walivaa mavazi yenye kufanana rangi, viatu, suruali za kubana na brauzi zenye kuonyesha sehemu kubwa ya migongo yao, huku wakiwa vichwa wazi.

Askari wenye dhamana ya kuhakikisha usalama unakuwepo chuoni hapo, waliwambia wanafunzi hao waondoke katika eneo hilo la chuo, kwa madai kuwa mavazi waliyovaa hayaendani na sehemu hiyo inayojihusisha kutoa elimu.

Katika siku za hivi karibuni Jordan imekuwa ikikabiliwa na maandamano ya kiraia wakidai uhuru katika mambo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment