TTCL

EQUITY

Thursday, June 27, 2013

JESHI LA POLISI TANZANIA LAJIBU MAPIGO ULINZI WA OBAMA

Tumejipanga vizuri ziara ya Obama - POLISI

NewsImages/6920558.jpg
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

JESHI LA POLISI nchini limesema limejipanga vilivyo kukabiliana na ugeni wa ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama wakati akiwa nchini na kuwatoa hofu wananchi.
Jeshi hilo limewataka watanzania wawe watulivu wakati Rais huyo akwia nchini na kuwaondoa hofu ambayo wengi imewaingia kutokana na ziara hiyo

Hayo yalisemwa jana na Msemaji wa Jeshi hilo Bi. Advera Senso, wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari

Amesema, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha kuwa kuna ulinzi mkali na madhubuti kwa muda wote wa ziara hiyo nchini,nakuwataka wananchi kuwa watulivu na atakayeonekana anakwenda kinyume atashughulikiwa kisheria.

Amewaomba wananchi kwua watulivu na kwa kwa yeyote atakayemuona mtu anafanya vitendo vya uharifu anaombwa aote taarifa kwa jeshi hilo ili kumdhibiti mtu huyo

Taarifa hiyo imesema Rais Obama anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi mwaka huu na nchi itaanza kupokea wageni kutoka nchini Marekani kuanzia wiki hiii

Hata hivyo wananchi wamekwua na maoni tofauti kuhusiana na ziara hii ya Rais Obama ambapo maoni hayo mengine ni hasi na mengine ni chanya

No comments:

Post a Comment