Wasomi wapinga kauli ya Rais Kikwete
Wamedai kuwa kuanzia Serikali ya Awamu ya Tatu
hadi hii ya nne zimekuwepo kauli za kupiga marufuku kashfa dhidi ya dini
nyingine lakini kukashifiana kumekuwa kukifanyika tena kwa uwazi bila
hatua kuchukuliwa.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti,
walitoa mifano ya kuwepo na mihadhara, CD, DVD na vipeperushi vya
uchochezi na kashfa dhidi ya dini lakini hakuna anayechukuliwa hatua.
Kwa kuwa mambo haya yamekuwa yakifanyika muda mrefu bila hatua kuchukuliwa wameshauri Polisi,wakuu wa mikoa,wilaya na usalama wa taifa wachukuliwe hatua kwa kushindwa kusimamia sheria na sasa amani ya nchi inaingia shakani.
Kwa kuwa mambo haya yamekuwa yakifanyika muda mrefu bila hatua kuchukuliwa wameshauri Polisi,wakuu wa mikoa,wilaya na usalama wa taifa wachukuliwe hatua kwa kushindwa kusimamia sheria na sasa amani ya nchi inaingia shakani.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk
Benson Bana amesema kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni kauli ya kisiasa na
alitakiwa kutoa tamko la kuwawajibisha watendaji wake pindi
wanaposhindwa kutekeleza wajibu wao.
Alisema vitendo hivi vyote vya machafuko ya
kidini vinafanyika hadharani huku wakuu wa mikoa,wilaya na Usalama wa
taifa wakishuhudia wakati jukumu la kulinda amani katika eneo husika ni
lao.
Naye Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama Cha Wananchi
(CUF), Julius Mtatiro anasema Serikali inayoongozwa na CCM haina uwezo
wa kutokomeza udini.
Katika hotuba yake ya kawaida ya kila mwisho wa
mwezi aliyoitoa Februari 28, mwaka huu, Rais Kikwete aliiagiza Polisi
nchini kukamilishe mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na
wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa
wengine.
Aliwataka wakuu wa mikoa nao kutoona ajizi katika hilo.
No comments:
Post a Comment