TTCL

EQUITY

Sunday, March 3, 2013

Mwanamke wa ajabu, mguu wake una uzito wa kilo 107


 

“Tatizo hili lilianza kuonekana toka nilivyozaliwa baada ya miguu yangu kuonekana ilikuwa ni mikubwa kuliko viungo vingine. Madaktari hawakujua haraka kwamba lilikuwa ni tatizo, hata hivyo walijidadisi sana. Hawakutaka mama yangu anione kwa wiki mbili. Hawakudhani kama nitaishi”
LANCASHIRE, Uingereza
JOPO la madaktari wamemwahidi mwanamke ambaye mguu wake unakua kila kukicha kuwa, wanamtafutia suluhu ya tatizo lake baada ya kupata ramani ya DNA yake.
Mandy Sellars, 38, hali yake kiafya imesababisha miguu yake kukua bila kukoma maisha yake yote.
Licha ya kuwa na tatizo hilo, Mandy alilazimika kukatwa mguu wake wa kushoto baada ya kuambukizwa virusi vya ‘septicaemia’.
Lakini baada ya miaka mitatu mguu wake huo ulianza kukua tena na mpaka sasa una uzito wa kilo 19.
Mandy hivi karibuni baada ya kupimwa maumbile yake hayo, madaktari hao waligundua kuwa ni binadamu wa kwanza kupatwa na maradhi hayo.
Hali hiyo inamsababisha, Mandy ashindwe kuzunguka na kusafiri sehemu mbalimbali, muda wote wa wiki hutumia akiwa nyumbani.
Akihitaji kusafiri hutumia kiti maalum kuweza kutembelea.
Madaktari walijaribu njia mbalimbali kuhakikisha kuwa wanasitisha hali hiyo, lakini mguu wake unaendelea kuongezeka, hadi sasa Mandy hana uwezo wa kutembea kutokana na uzito wa miguu yake.
“Mimi sioni kama kuna uwezekano wa kusimamisha hali hii,” alisema Mandy anayeishi huko Huncoat, Lancashire nchini Uingereza, Ninahitaji kubadili haya maisha nimeyachoka, natamani kuachiliwa kutoka hapa na nitoke nje mwenyewe nikaishi huko.”anasema.
Hali hiyo ya Mandy inaweza kupata uwezekano wa kupona baada ya wanasayansi kutoka, Chuo Kikuu cha Cambridge kuamua kuchukua nafasi ya kujaribu kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
Mwaka jana Dk Robert Semple alichukua DNA ya Mandy kutoka katika sampuli ya tishu ya damu yake kwa ajili ya kupima tatizo alilonalo.
Hata ivyo utafiti huo ulibaini kuwa alikuwa na machafuko ya kipekee.
“Mimi ni mtu wa kwanza katika dunia kupatwa na tatizo hili ambalo mpaka sasa bado halijapatiwa jina,” alisema Mandy wakati akihojiwa na televisheni ya ITV kwenye kipindi cha This Morning.
“Nilipendekeza kwa Dk Semple kuwa ugonjwa huu auite Sellars Syndrome!” alisema Mandy huku akisisitiza kuwa katika majibu ya daktari Semple na timu yake walipendekeza apatiwe matibabu ya jeni.
Dk Semple anasema: “Nilianza kuchukua vipimo mwezi Septemba mwaka jana, na lengo lilikuwa ni kusitisha ukuaji wa miguu yake. Awali ya wote walianza kwa kuchukua vipimo vya DNA” alisema Semple.
Mandy anasema alikuwa amekata tamaa kutokana na hali yake, lakini utafiti wa Dk Semple ulimfanya mpaka sasa aweze kujua kuwa atapatiwa suluhu ya tatizo lake.

No comments:

Post a Comment