TTCL

EQUITY

Wednesday, October 9, 2013

DIAMOND; "NAMPENDA SANA PENY, SINA HABARI NA WEMA... ACHENI POROJO"


Baada ya kusambaa kwa taarifa za Diamond Platnums kurudiana na Wema Sepetu, Diamond kupitia website yake leo ameandika…. “kumekuwa na Uvumi na habari nyingi sana Mitandaoni na kwenye Media tofauti kwamba mimi na Wema Sepetu tuna mahusiano ya Kimapenzi, kitu ambacho sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye Account yangu ya Instagram?..

‘Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano basi msizungumze ama Kushiriki kwa chochote? Futeni huo uzamani na mbadilike, inamaana mnapenda kuona watu wanauadui… ni muda wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania na si kuekeana chuki zisizo na faida, I REAL LOVE MY PENNY,SIJARUDIANA NA WEMA’ – Diamond Platnumz

No comments:

Post a Comment