TTCL

EQUITY

Monday, February 6, 2017

Sakata la ‘Unga’: Rais Magufuli Apigilia Msumari Vita ya Makonda Dhidi ya Watumiaji na Wauzaji wa Dawa za Kulevya


Rais Magufuliakizungumza baada ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi, Kamishna wa Magereza, Mnadhimu Mkuu na Mabalozi.
Siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitosa kwenye vita ya madawa ya kulevya kwa kuagiza wasanii, wafanyabiashara na askari  wanaodaiwa kuhusika na utumiaji na biashara ya madawa ya kulevya wajisalimishe kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano, huku wengine wakiwa tayari wameshaanza kuchukuliwa hatua, Rais Magufuli amempongeza kwa hatua hiyo na kumtaka aendelee kuwakamata wahusika wote.

Rais Magufuliakizungumza baada ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi, Kamishna wa Magereza, Mnadhimu Mkuu na Mabalozi.
Raia Magufuli, amesema anafurahishwa na namna Makonda anavyofanya kazi hiyo na kutaka aendelee kuwakamata, bila kujali umaarufu au cheo cha mtu na kuwataka viongozi wengine kuungana naye kuhakikisha wahusika wote wa biashara ya madawa ya kulevya, wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria. Akaongeza kuwa watumiaji wakikamatwa, wabanwe ili wawataje wanaowauzia mpaka kuwafikia wauzaji wakubwa.
Rais Magufuli ameyazungumza hayo katika hafla ya kuapishwa kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali James Mwakibolwa pamoja na mabalozi wa Tanzania nchini Ufaransa na DRC.

Pia Rais Magufuli amemuagiza kaimu jaji mkuu wa Tanzania, kuhakikisha kesi za madawa ya kulevya, zinasikilizwa haraka na kutolewa hukumu ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaoshiriki kwenye biashara hiyo inayomaliza nguvu kazi ya taifa.Rais Magufuli alikumbushia kesi ya mfanyabiashara wa madawa ya kulevya aliyekamatwa Mtwara, Shikuba ambaye licha ya kukamatwa siku nyingi zilizopita, bado hajapandishwa mahakamani na kuitaka idara ya mahakama, kushughulikia suala hilo haraka.
Mabli na hivyo, Rais Magufuli amempongeza IGP Mangu kwa kuwasimamisha kazi Askari 12 wanaotuhumiwa kujihushisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa vita hiyo siyo ya RC Makonda pekee bali ni ya Watanzania wote.

 ALICHOKISMEA RAIS MAGUFULI
 

Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni- Rais Dkt
Najua IGP kuna watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu dawa za kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa ni IGP- Rais Dkt
Ombi langu ni Tanzania ya viwanda ionekane kwenye majeshi yetu, haiwezekani hadi leo tunaagiza sare kutoka nje ya nchi- Rais Dkt
Kuna mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa mahakamani, its too much- Rais
Hawa wakubwa wakubwa tuwashughulikie badala ya kusumbuka na hawa wadogo wadogo. -Rais

Nataka wafungwa wawe wanafanyakazi, ukiwafunga tu na kuwapa chakula ndio sababu wanarudia makosa kila siku wakitoka- Rais Dkt
Mfungwa aliyefungwa miaka mingi afanye kazi nyingi zaidi kulisaidia taifa, kwani tuna miradi mingi kama barabara na reli.
Usije ukateuliwa kwenda kufanya kazi kwenye Tume ya Utumishi harafu nikakuta kuna watumishi hewa –
IGP nakuagiza kamata watuamiaji wote wa dawa za kulevya hao watakwambia wanapozipata, haiwezekani ziuzwe kama njugu- Rais Dkt
Vita ya dawa za kulevya si ya Paul Makonda peke yake, ni ya watanzania wote, naviagiza vyombo vyote vishirikiane- Rais Dkt
Haiwezekani vijana tunaotarajia kupawa nchi kesho wanatumia dawa alafu kuna watu wanapita na kutamba kwa utajiri- Rais Dkt
Najiskia vibaya sana kusikia chombo cha ulizni kinatuhumiwa kwa tuhuma yoyote. –

Sikutaka kumchagua Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kabla sijaenda Ethiopia sababu nilijua watasema Mwamunyange ametumbuliwa- Rais Dkt
Tumewateua mkalinde mipaka yetu, kusiwe ma magendo magendo huko –
Maslahi ya wanajeshi tunayashughulikia, kafanyeni kazi mkijua mko pamoja na serikali, tunawaamini sana –
Mwenyezi Mungu awabariki ninyi nyote, mkatende kazi kama tuklivyowaagiza. –
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa na Kamanda Sirro katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam amezungumza na wanahabari kuhusu oparesheni ya kusaka wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya kwa mkoa wake. 

Mambo  aliyoyasema Paul Makonda leo ni kutoa siku kumi kuanzia kesho February 7, 2017 kwa Wenyeviti wa mtaa, Wazazi na Watumiaji na Wafanyabiashara.
Natoa siku 10 kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es Salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya.
Natoa siku 10 kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto anatumia dawa za kulevya na unaishi nae, njoo utoe taarifa….. tukikukamata baada ya siku kumi na mwanao anahusika tutaamini na wewe ulikua sehemu ya kumfanya mtoto wako atumie dawa za kulevya.
Natoa siku 10 kwa Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za kulevya, waje wenyewe Polisi kwa kamishna, kama umekua ukifanya biashara ya dawa za kulevya na umeacha njoo Polisi, nguvu tunayo, uwezo tunao…. hakuna kiunga tutashindwa kufika, hizi kelele nyingine zinatupa hamasa. Alisema Makonda.

No comments:

Post a Comment