TTCL

EQUITY

Tuesday, May 10, 2016

Serikali kuboresha huduma ya afya

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI Selemani Jaffo amesema serikali imeandaa mpango wa upatikaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya chini, ili kupunguza msongamano katika hospitali za rufaa hapa nchini.
 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Selemani Jaffo
 
Jaffo ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Segerea, Bona Kalua aliyetaka kujua mpango wa  serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa manispaa ya Ilala jijini Dar Es Salaam.

Amesema wana mpango wa kuinua hadhi ya baadhi ya zahanati kuwa vituo vya afya vitakavyokuwa na uwezo wa kutoa huduma zaidi za afya katika jamii.

Kuhusu tuhuma zinazowakabili askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania – JWTZ, za kuwanyanyasa wavuvi katika maeneo ya Kigamboni na Kunduchi jijini Dar Es Salaam Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi ameliambia bunge kwamba taarifa hizo hazijamfikia.

Amesema ikibainika kuna askari waliofanya vitendo hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kama raia mwingine yeyote bila kujali ni askari.

No comments:

Post a Comment