TTCL

EQUITY

Tuesday, May 10, 2016

Mchakato wa uchaguzi waendelea DRC

Kiongozi wa upinzani aliyetangaza kugombea urais katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo – DRC, Moise Katumbi amekanusha tuhuma za kuwatumia mamluki wa kukodiwa kuwa walinzi wake.
 
Moise Katumbi

Katumbi alifika mahakamani jana baada ya kutangaza wiki iliyopita kuwa atapeperusha bendera ya vyama saba vya upinzani katika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba nchini DRC.

Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Katumbi wakati alipofika mahakamani mjini Lubumbashi.

Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu limesema tuhuma dhidi ya mgombea huyo wa upinzani zinaonekana kuchochewa kisiasa.

Rais Joseph Kabila aliyeko madarakani hajatangaza kama atagombea katika uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment