TTCL

EQUITY

Saturday, April 16, 2016

Swabrina Ghalibu: Kazi ni kazi ilimradi iwe na uhalali

Wengi wa vijana wa mjini wamekuwa wakichagua kazi, lakini hali ni tofauti kwa bidada huyu Swabrina Ghalibu (19), unaambiwa ni mwanamke wa kwanza mhudumu wa Mochuari pale Hospitali ya Tumbi (Kibaha) huku wengi wakimsifia kuwa ni 'Jembe

 
SWALI: Wewe mbona huogopi
SWABRINA: Ni kazi ambayo ninaipenda. Sikushawishiwa na mtu na hivyo naifanya kwa moyo mmoja bila ya woga.
SWALI: Marafiki zako wanakuchukuliaje, hasa wale mnaoishi nao Mlandizi na hata wale mliomaliza nao shule ya sekondari?
SWABRINA: Ki-ukweli wananiogopa sana! Kuna waliowahi kuja hapa Mochuari walikuwa wamefiwa. Waliponikuta hapa, walishangaa sana. Waliniogopa na kusema mimi sio mtu wa kawaida.
Una neno gani la kumwambia dada huyu mwenye ujasiri uliowashinda wanaume wengi?