TTCL

EQUITY

Saturday, April 16, 2016

Katimba kuwasilisha hoja kutatua tatizo la ajira

Mbunge wa viti maalumu kupitia vijana wa CCM, Mkoani Kigoma, Bi. Zainabu Katimba ameendaa hoja binafsi kupeleka bungeni ili kuishinikiza serikali kutatua tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo vya ufundi na elimu ya juu nchini.


Akiongea mjini Kigoma Mbunge huyo wa viti Maalumu amesema kuwa hoja yake inalenga kushinikiza serikali itunge sera ya ulazima kwa taasisi mbalimbali kuajiri wahitimu wa elimu ya juu na ufundi ili kuwapatia mafunzo na hivyo kupata uzeofu ambao umekua kikwazo wakati wa kutafuta ajira.

Bi. Zainabu amesema vijana wengi nchini wanakumbana na tatizo la kuambiwa kuwa na uzeofu katika kazi kwa kipindi kisichopungua miaka kadhaa hali inayofanya wahitimu wengi kuelea kusota mitaani.

Vilevile ameongeza kuwa nchi nyingi zimeweza kuandaa sera hizo ikiwemo nchi jirani za Kenya na Uganda na kusema endapo sera hiyo itafinyiwa kazi nchini basi tatizo hilo linaweza kupungua kama si kumalizika kabisa.

Aidha amesema kuwa licha ya kupata mafunzo hayo ambayo watayapata kupitia taasisi hizo pia yataweza kufungua soko la ajira kwa vijana wengi ndani na nje ya nchi.
Mkuu wa Idara ya UVCCM, na Mbunge wa viti maalumu kupita vijana Mkoani Kigoma, Zainab Katimba akiongea wakati wa kufungua kikao cha vijana.

No comments:

Post a Comment