TTCL

EQUITY

Wednesday, March 2, 2016

SERIKALI YAKUMBUSHWA KUVIANGALIA VITUO VYA KULEA WATOTO YATIMA NA WASIOJIWEZA

SERIKALI ya Awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli imeombwa kuviangalia kwa ukaribu vituo vya kulelea watoto yatima na wasiojiweza kwa kuvipatia ruzuku ili viweze kujiendesha vyenyewe tofauti na hivi sasa vinategemea misaada kutoka kwa wasamaria wema.
watoto wakiwa katika picha ya pamoja
Rai hiyo ilitolewa na Bi. Jenipher  Massawe mmoja wa walezi wa watoto wenye ulemavu wa akili na wasiojiweza wa Kituo cha Building Caring Community (BCC) alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wetu, katika mmoja ya vituo 11vilivyopo chini ya kanisa la KKKT usharika wa Moshi Mjini.
Bi. Jenipher  Massawe akizungu na watoto
Watoto waliopo kituoni hapo mara nyingi hupelekwa baada ya kutambuliwa na viongozi wa serikali ya mtaa, pamoja na barua ya utambulishi wao kutoka kwa kiongozi wa kiroho, ambapo wengi wao hutoka katika kaya masikini. aidha baadhi ya watoto hupelekwa na walezi wao baada ya baba au mama kufariki dunia hivyo humsaidia kulea, kuwapatia mafunzo na mazoezi ya viungo, tiba, pamoja na lishe, ambapo huwawapeleka kutwa na kuwachukua jioni. Pia mtoto anapofikia umri wa kujitambua na kufika umri wa kuanza masomo kituo kina hakikisha kumsaidia mtoto anakwenda shule. alisema

Aliongeza kusema, kituo kimekua kikitoa mikopo ya gharama nafuu, yenye riba ya 6%  kwa wazazi wa watoto wote wenye ulemavu, na kufanya msako wa nyumba kwa nyumba ili kufichua watoto wenye ulemavu waliofungiwa ndani na kutoa mafunzo/ elimu kwa jamii kuhusu madhara ya kuwaficha watoto wao.
Aidha alimalizia kwa kutoa wito kwa serikali ya awamu  ya tano kuhakikisha kuwa inavikumbuka vituo vyote vya kulea watoto yatima, na wasiojiweza katika kuwapatia ruzuku na miasaada mbalimbali kwakua vimekuwa vikifanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii, hususa kaya masikini na zenye watoto walemavu, ambapo wengi wao huenda wangekuwa ombaomba na watoto wa mitaani.

No comments:

Post a Comment