Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (UWERA) imesema kuwa imepokea maombi kutoka Shirika la Umeme nchini ili kupunguza gharama za umeme nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi na kueleza kuwa Februari, 24 UWERA ilipokea maombi kutoka TANESCO ambayo inaelezea mabadiliko ya bei ya umeme kwa miaka miwili kuanzia April, 1.

DSC_0828
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi akizungumza na waandishi wa habari.

“TANESCO wamewasilisha ombi husika kulingana na kifungu NA. 24(2) cha Sheria ya Umeme Naa. 131 kinachoitaka mamlaka kufanya mabadiliko ya bei zinazotozwa kwa mtoa huduma mara moja kila baada ya miaka mitatu,
“Pendekezo la wastani wa badiliko la umeme ni asilimia 1.1 kuanzia Aprili, 1 mwaka huu na asilimia 7.9 kuanzia Januari, 1,  2017,” alisema Ngamlagosi.
Alisema kuwa mujibu wa kifungu Na. 19(2) (b) cha sheria za EWURA, sura NA. 414 wanatakiwa kuanzisha mchakato wa kupata maoni ya wadau ili kujua uhalali wa maombi ya mapendekezo ya bei za huduma iliyoyapokea kutoka TANESCO.
Aliongeza kuwa mkutano wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau utafanyika Machi, 4 jijini Sa res Salaam.