TTCL

EQUITY

Wednesday, March 9, 2016

Balozi Mahiga ala kiapo cha utii katika Bunge la Afrika Mashariki

maiga2
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) amekula kiapo cha utii mbele ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, akiwa kama Waziri anayehusika na Shughuli za Ushirikiano wa Afrika Masahiriki kutoka Tanzania. Tukio hilo la kuapishwa kwa Waziri Mahiga limeshuhudiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndungai, Hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakishuhudia Balozi Mahiga akila kiapo (hayupo pichani).
Sehemu ya watumishi kutoka Serikalini wakifuatilia tukio hilo la uapisho. Mstari wa nbele katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga.
Sehemu nyingine ya viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, na kulia ni Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb.) wa kwanza kushoto, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Daniel Kidega    na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndungai kwa pamoja wakiimba wimbo wa Afrika Mashariki kabla ya Kuapishwa kwa Waziri Mahiga (hayupo pichani). 
Waheshimiwa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki nao wakiimba Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Shughuli za Kibunge zikiendelea  mara baada ya kumalizika kwa tukio la Uapisho wa Balozi Mahiga.

No comments:

Post a Comment