TTCL

EQUITY

Wednesday, January 13, 2016

Waziri wa Afya avipandisha hadhi vituo viwili vya afya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, UMMY MWALIMU amevipandisha hadhi vituo viwili vya afya vya MJIMWEMA na MADABA 
 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, UMMY MWALIMU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, UMMY MWALIMU amevipandisha hadhi vituo viwili vya afya vya  MJIMWEMA na MADABA wilayani  SONGEA mkoani RUVUMA, na kuwa hospitali ya wilaya hiyo.
Waziri MWALIMU ametangaza hatua hiyo mkoani RUVUMA wakati wa uzinduzi wa mpango wa  huduma za matibabu zinazotolewa na madaktari bingwa uliofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya - NHIF.
Amesema serikali itaziwezesha hospitali hizo kutoa huduma ya afya kulingana na hadhi stahiki.
Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa RUVUMA, Dkt. PHELIS NYIMBI amesema hospitali hiyo inakabiliwa na uhaba wa madaktari.

No comments:

Post a Comment