TTCL

EQUITY

Wednesday, January 13, 2016

Samatta ataka mipango ya kuimarisha Taifa Stars

Nahodha mpya wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania TAIFA STARS MBWANA SAMATTA amesema kunahitajika mipango madhubuti ambayo itaimarisha timu hiyo na sio kuendelea kujaribu kama inavyofanyika hivi sasa
Nahodha mpya wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania TAIFA STARS MBWANA SAMATTA
 
Nahodha mpya wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania TAIFA STARS MBWANA SAMATTA amesema kunahitajika mipango madhubuti ambayo itaimarisha timu hiyo na sio kuendelea kujaribu kama inavyofanyika hivi sasa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na TBC, SAMATTA amesema TAIFA STARS imekuwa ikipanda na kushuka na bado haijafika kwenye ubora unaohitajika.

SAMATTA amesema umefika wakati wa kuwa na mpango mkakati wa kuipandisha timu hiyo kwa muda mrefu kama vile kuwekeza kikamilifu kwenye soka la vijana.

TAIFA STARS inayofundishwa na CHARLES BONIFACE MKWASA ina kibarua kigumu hivi sasa cha michuano ya awali ya kufuzu kwa michuano ya MATAIFA ya AFRIKA baada ya kutolewa kwenye michuano ya awali ya kuwania kuingia hatua ya makundi ya kufuzu kwa kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment