TTCL

EQUITY

Wednesday, January 13, 2016

David Beckham kwenye hii tuzo nyingine ya heshima…

Ustaa wa David Beckham si tu kwenye soka..baada ya kustaafu soka amekua akishiriki katika mambo mbalimbali ikiwemo mitindo pamoja na kushiriki shughuli za kijamii.
Jana Shirika linalosimamia haki za watoto UNICEF limemzawadia tuzo ya heshima staa huyo baada ya kuonyesha mchango mkubwa katika kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Sherehe za yuzo hizo zilifanyika jana huko Beverly Hills na kuhudhurikiwa na baadhi ya mastaa akiwemo Mariah Carey ambaye alikua akitoa burudani, Selena Gomez pamoja na Nicole Kidman.

mari
Mwanamuziki Mariah Carey akitumbuiza

sele
Selena Gomez

Beckham alifanikiwa kupata tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kushiriki kwenye shughuliza jamii ikiwemo kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kupitia miradi yao.

ing

No comments:

Post a Comment