Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
HAMIDA HASSAN NA GLADNESS MALLYA, IJUMAA
DAR ES SALAAM: Baada ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma kufunga ndoa na mheshimiwa Sadifa Juma, anadaiwa kutengwa na wasanii wenzake wa Bongo Muvi hasa wale waliokuwa karibu naye katika zoezi la kumchangishia fedha za matibabu aliyokuwa akitarajia kwenda kuyafanyiwa nchini India.
DAR ES SALAAM: Baada ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma kufunga ndoa na mheshimiwa Sadifa Juma, anadaiwa kutengwa na wasanii wenzake wa Bongo Muvi hasa wale waliokuwa karibu naye katika zoezi la kumchangishia fedha za matibabu aliyokuwa akitarajia kwenda kuyafanyiwa nchini India.
Sosi wa ndani ya Bongo Muvi alilinyetishia Ijumaa kwamba, baadhi ya
mastaa walifikia uamuzi kufuatia kukasirishwa na kitendo cha Wastara
kuolewa ghafla bila kuwashirikisha wao.
“Wasanii wamemkasirikia sana Wastara na ninavyokwambia kwa sasa kimenuka kwani hawataki hata kumsikia.
“Wanamshangaa
kuolewa wakati anaumwa na alikuwa akiomba msaada hivyo wamemtenga na
wamesitisha michango yake,” kilifunguka chanzo hicho.
Ilielezwa kwamba, aliyekuwa akiongoza ishu ya kumchangishia ni Rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba aliyejitolea
kuandika barua na kuipeleka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo kwa ajili ya kuomba msaada wa matibabu ya mguu wake nchini India
lakini walisitisha mara moja zoezi hilo baada ya ndoa hiyo.
Mwakifwamba alipoendewa hewani na kufikishiwa ishu hiyo alisema:
“Nilifuatwa na kaka wa Wastara, akaniomba kuwa dada yake anaumwa sana,
anahitaji kwenda kwenye matibabu India, nikaamua kumuandikia barua ya
kumuombea msaada wizarani.
“Barua hiyo niliipeleka kwa katibu mkuu wa wizara hiyo, Profesa
Elisante Ole Gabrielleo. Alipoipokea aliniambia kuwa ataishughulikia
iende Wizara ya Afya kwa ajili ya matibabu hayo haraka na mchakato
ulikuwa unaenda vizuri.
“Ilipofika jioni nikashangaa kuona mitandaoni kuwa Wastara anaolewa,
nikaona nimpigie haraka katibu mkuu kwani barua yangu ilisema kuwa
Wastara ni mgonjwa sana ambaye anahitaji matibabu ya haraka kwa hiyo
kitendo cha kufunga ndoa kilinishtua kwani sikulitambua.
“Baada ya kumweleza katibu mkuu huyo alisema kuwa kwa sababu ameolewa
na mbunge kuna taratibu zao azifuate hivyo tukaishia hapo.”
Kwa upande wake Wastara alifunguka mambo mazito ya kusikitisha:
“Nikiongea sasa nitaonekana najitetea lakini wasanii wenzangu wajue kuwa
niliamriwa na mume wangu, niliwatumia ujumbe kwenye makundi yetu na
kuwaeleza kuwa naolewa.
“Hata hivyo, ndoa haikuwa imepangwa kwa siku hiyo kama wanavyodhani
ila baada ya mimi kuwa na hali mbaya, Sadifa aliwaomba ndugu zangu na
kuwaambia kuwa anataka anioe hivyohivyo ili anihudumie kwa sababu
tulipanga ndoa baada ya mimi kutoka kwenye matibabu.
“Wasanii ni watu wa kulaumu tu, ila mimi naumwa sana, Mungu akipenda
nitakuwa India ‘soon’, nitafanyiwa matibabu na anayetaka kunichangia
nitamshukuru.”
No comments:
Post a Comment