TTCL

EQUITY

Friday, January 15, 2016

Asilimia 10 ya wanafunzi, wamefeli kidato cha 2

Baraza la mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili uliofanyika Novemba 2015.

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa baraza la mitihani taifa Dkt. Charles Msonde amebainisha kuwa jumla ya wanafunzi 363,666 sawa na asilimia 91.66 walifanya mtihani wa upimaji wa kitaifa.




Kati ya hao waliofanya, wasichana walikuwa 184,895 sawa na asilimia 92.63 na wavulana 178,771 sawa na asilimia 90.68 ambapo jumla ya wanafunzi 33,104 sawa na asilimia 8.34 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro na ugonjwa.

Matokeo yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 324,068 sawa na 89.12% wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu ambapo wasichana ni 164,547 sawa na 89.00 na wavulana 159,521 sawa na 89.24%. Aidha wanafunzi 39.567 sawa na 10.88% wameshindwa kupata alama za kuendelea na kidato cha tatu.
Matokeo
Dkt Msonde amesema jumla ya wanafunzi 155,667 sawa na asilimia 42.80 waliofanya mtihani wa upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili (FTNA) mwaka 2015 wamepata ufaulu mzuri wa madaraja yaani Distinction, Merit na Credit.
Aidha Dkt.Msonde amesema kiwango cha ufaulu kimepanda katika masomo msingi ya Kiswahili, Commerce na Chemistry umepanda huku katika masomo ya Sayansi ya Fizikia, Biologia pamoja na Hisabati kikionekana kushuka hali inayohitaji juhudi za ziada.

Baraza la mitihani limewataka walimu pamoja na maofisa elimu wa wilaya pamoja na mikoa kufuatilia kwa ukaribu ufundishaji katika shule zilizofanya vibaya ili kuinua kiwango cha ufaulu na kubainisha kuwa suala la udanganyifu limeendelea kujitokeza

Katika upangaji wa matokeo hayo ambao umezingatia wastani wa point (GPA) ambapo A=5, B+4, B=3, C2, D=1, E=0.5 umeonyesha kuwa shule zilizotoa 10 bora ni shule 3 mkoa wa Mwanza, 4 Dar es salaam, 2 Iringa na 1 Mbeya. Shule 10 zilizofanya vibaya ni shule 5 Mkoa wa Tanga,3 Mtwara,1 Dar es salaam na 1 Lindi.
Bofya hapa kuangalia matokeo====>bit.ly/1n5HK8w

No comments:

Post a Comment