Baadhi ya wananchi na abiria kutoka mikoa ya GEITA, KAGERA
KIGOMA, MWANZA na SHINYANGA wanaotumia barabara ya KIGOMA hadi
NYAKANAZI mkoani KAGERA, wameiomba serikali kuongeza kasi ya ujenzi wa
barabara ya kilomita 50 kwa kiwango cha lami kuanzia eneo la KIDAHWE
hadi KASULU mkoani KIGOMA, ili kupunguza adha ya usafiri katika
kipindi cha mvua za masika.

Wakizungumza katika mahojiano na TBC wananchi hao wamesema katika
kipindi hiki cha masika barabara hiyo imekuwa haipitiki kwa urahisi na
kusababisha kukwama kwa magari kadhaa ya abiria na wakati mwingine
abiria hulazimika kulala njiani.
No comments:
Post a Comment