1) Toa shukrani.
Kila siku ukiamka asubuhi Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kuamka
salama na mwenye afya. Kitendo cha kushukuru kitakufanya ujione una
jambo la kushukuru na kuwa wewe ni mwenye bahati. Kuna mambo mengi sana
ya kushukuru, kama vile afya yako, nyumba unayolala, gari unaloendesha,
chakula unachokula, mpenzi uliyenaye n.k. Fikiria mambo matano ya
kushukuru kila siku asubuhi na utajiongezea furaha maishani mwako.
2) Amka mapema
Uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha boston huko Marekani
kinaonyesha kuwa watu wanaoamka mapema wanakuwa na furaha zaidi kuliko
watu wanaochelewa sana kuamka. Kama unaweza ni vyema kuamka saa 11 au 12
asubuhi.
3) Panga ratiba ya siku nzima


Umeshawahi kurudi nyumbani jioni na kujiona kama siku yako imepotea
bure na hamna cha maana ulichokifanya? wakati mwingine inawezekana
kabisa kuwa umefanya kazi nyingi lakini kwasababu hukupanga ni nini
utafanya siku hiyo unajiona kuwa hujafanya chochote. Ni vyema kuandika
list ya vitu unavyopanga siku nzima, mwisho wa siku ukifika unaangalia
list ya vitu ulivyovifanya na kuvimaliza, utajipongeza na kulala vizuri
ukijua siku yako imekuwa ya mafanikio.
4)Fanya mazoezi
Kufanya mazoezi kunasaidia kujisikia vizuri, kuwa na afya njema,
kulala vizuri, kupendezesha ngozi na kujiepusha na magonjwa mbali mbali
hasa yale yanayosababishwa na unene.
Kwa wale waliozoea kupiga desh asubuhi huu ndio muda muafaka kuacha
hiyo tabia. Umeshasikia kuwa “breafast is the most important meal of the
day”. Ukiacha tumbo bila chakula muda mrefu unajiweka kwenye hatari ya
kupata ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Kumbuka wengi wetu huwa tunakula
chakula cha jioni saa mbili usiku, ikifika saa mbili asubuhi tayari ni
masaa 12 hujaweka kitu tumboni, ukipiga desh breakfast mpaka saa saba
mchana hayo ni masaa 17 umekaa bila kuweka kitu tumboni. Faida nyingine
ya kula breakfast ni kukupa nguvu na hujisikii umechoka choka ukifika
kazini. Ukiona mtu ameingia kazini amenuna, muulize kama amekunywa chai
na jibu lake litakuwa ni hapana.
6) Mfanyie mtu yeyote jambo jema


kumfanyia mtu jambo jema inakufurahisha wewe na pia inamfurahisha mtu
ambaye umemfanyia jambo jema, Na sio lazima huyo mtu awe ni ndugu yako
au mtu aunayemjua. Mambo ya kufanya kumfurahisha mtu ni mengi sana,
nitakupa mfano wa mambo machache ambayo mimi mwenyewe huwa nafanya.
Mambo hayo ni kama kumfungulia mtu mlango, Kumsaidia omba omba
barabarani, kumnunulia rafiki yako lunch, kumrushia bibi yako hela ya
sukari, kumpa mtu lift ya gari n.k Hakikisha kila siku unamfanyia mtu
jambo jema na itakuongezea wewe furaha.
7) Sikiliza muziki wenye furaha (up beat music)


Utakuta mtu anaingia kwenye gari asubuhi anaweka wimbo wa majonzi
jinsi anavyo-m-miss bebi wake au nyimbo nyingine tu za huzuri, mwisho
wake utaishia kujisikia mwenye huzuni. Sikiliza nyimbo zilizo changamka
na utajisikia umechangamka na mwenye furaha.
8) Mpigie simu mtu na umwambie namna unavyompenda


Kusema neno nakupenda ni ngumu kidogo kwenye jamii yetu. Lakini
jitahidi kusema nakupenda mara kwa mara, ukiongea na mke wako , mtoto
wako, bibi yako waambie unawapenda. Kuna miujiza katika neno nakupenda
na ukilitumia vizuri utaiona hiyo miujiza.
Je kuna jambo lolote ambalo wewe unafanya linakuongezea furaha..kama lipo acha comment hapo chini.

No comments:
Post a Comment