TTCL

EQUITY

Wednesday, January 13, 2016

Wanufaika mikopo elimu ya juu watakiwa kurejesha

Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini imesema kuwa imeshatoa sh. billioni 459 kwa wanafunzi 122,486 kwa mwaka wa masomo wa 2015/16 ambapo imeelezwa ni kiwango cha juu zaidi kushinda miaka iliyopita.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo Omega Ngole ambapo amesema kuwa mwaka huu wa masomo 2015/16, bodi hiyo imetoa mikopo kwa wanafunzi wengi zaidi tofauti na mwaka wa masomo 2014/15 ambapo jumla ya wanafunzi 99,069 walipata mikopo ya jumla ya sh. Bilion 341.
Aidha Bw. Ngole amewataka wanufaika wote wa mikopo kuanza kurudisha mikopo kwa wakati kabla hawajaanza kulipishwa na faini
Ngole ameongeza kuwa waajiri wote wanawajibika kisheria kuorodhesha majina ya waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa mikopo pamoja na kuwakata 8% ya mishahara yao au 50,000/= kwa ajili ya marejesho ya mikopo yao.
wakati huo huo bodi hiyo imesema kuwa imekusanya sh. Billion 33.8 toka 2014 mpaka Desemba 2015 kutoka kwa wanufaika ambao wameanza kurejesha mikopo yao.

No comments:

Post a Comment