Kampuni ya BrighterMonday
ambayo ni tovuti namba moja ya ajira nchini Tanzania. Leo hii imezindua
kituo kipya ambacho kitatumika kwa ajili ya huduma ya mawasiliano na
wateja ambao ama ni watafuta ajira wapya au wanataka kubadili ajira.
Akizungumza wakati wa hafla ya kifungua kinywa Bwana Lugendo Khalfan, Meneja Masoko wa Kampuni ya BrighterMonday Tanzania
alisema kwamba changamoto kubwa nchini Tanzania ni kuwa kuna watafuta
ajira wengi sana kuliko nafasi za ajira zilizopo sokoni, hivyo kwa
kupitia kituo hiki itawarahisishia watafuta ajira kuongeza nafasi ya
kupata ajira kiurahisi na huduma zote ni bure.
Naye Bi. Eva Slootweg, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BrighterMonday amekielezea kituo hicho cha ajira ambacho kipo katika tovuti ya kampuni hiyo ambayo ni www.brightermonday.co.tz kuwa kina mfumo wa kuchambua maombi ya kazi mpaka kupata wachache wenye kukidhi viwango.
Kwenye
suala la upatikanaji wa watu wenye vigezo, utendaji mzuri, mahusiano
kazini na ujuzi katika uongozi pamoja, kampuni ya Brighter Monday ina
uwanja mpana ambao unakwenda sambamba na mabadiliko yaliyoko katika
sekta ya ajira ambayo si tu inatilia mkazo uwezo wa utendaji kazi na
ufanisi wa mwombaji ajira bali ni kwa namna gani mwomba ajira anaendana
na utamaduni wa taasisi husika.
Bi
Sabiha Monji, Mkurugenzi Mtendaji wa Shugulika Recruitment, alisema
mojawapo ya changamoto wanayokutana nayo hapa Tanzania ni kukosa umakini
kwa baadhi ya watafutaji ajira, “wengine wanashindwa kufika katika
usaili bila hata kutoa taarifa”. Katika utafutaji kazi katika mtandao,
Bi Sabiha alidokeza kwamba Tanzania kwa sasa ina watafuta ajira zaidi na
zaidi wanaotafuta kupitia mtandao, hivyo kuna kuna ongezeko la
watumiaji mtandao katika kutafuta ajira.
Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya waajiri 3000 kutoka sekta mbalimbali huajiri kupitia BrighterMonday.
Kampuni
ya BrighterMonday inafahamu changamoto zinazowakabili wadau wake hivyo
hutoa ufumbuzi unaokidhi matakwa ya mwajiri kwa kumpatia mwajiriwa
anayewafaa. Kutokana na uzoefu wa muda mrefu na kutokana na maoni kutoka
kwa wateja, na kwa ubunifu wameweza kuongoza soko la ajira nchini.
Kampuni ya BrighterMonday inadhamiria
kuendelea kuwashirikisha wadau wake kwa njia ya mijadala ya kiuongozi
ili waelewe changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya ajira Tanzania
na kutoa suluhisho kwa ubunifu na mikakati iliyo bora kama mshirika na
kampuni namba moja ya ajira nchini.
Brighter Monday ni nini?
BrighterMonday
Tanzania ni kampuni kubwa ya ajira mtandaoni, yenye watafuta ajira bora
kuliko kampuni yoyote. Kwa nia ya kuwarahisishia watafuta ajira,
tumeshirikiana na waajiri mbalimbali kuhakikisha kuwa katika upatikanaji
wa ajira kirahisi Zaidi, na ni daraja kati ya soko la ajira na waajiri.
BrighterMonday iko chini ya mwamvuli wa makampuni ya One Africa Media
(OAM), kampuni kubwa ya biashara za mtandaoni barani Africa. OAM
inashughulika na safari za kiutalii mtandaoni, magari na ajira katika
maeneo mbali mbali Afrika.
No comments:
Post a Comment