Mama mmoja Mkoani Dodoma anatuhumiwa kumuozesha
mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 (jina linahifadhiwa) kwa mahari ya
shilingi laki sita pamoja na ng’ombe wanne.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Tukio
hilo lilitokea jana katika Mtaa wa Chikole, Kata ya Msalato katika
Manispaa ya Dodoma ambapo mama huyo aliyefahamika kwa jina la Melea
Mazengo ameamua kumuozesha binti yake huyo kwa kijana mmoja
aliyefahamika kwa jina moja la Juma ambaye naye ni mkazi wa mtaa huo.
Hata hivyo mpango huo wa ndoa ulitibuliwa na mwenyekiti wa mtaa huo,
Nashoni Chinywa ambaye baada ya kupata taarifa za ndoa hiyo aliamua
kuita polisi ili kuivunja.
Akizungumzia tukio hilo mama mzazi wa mtoto huyo, Mdala Mazengo
amesema kuwa aliamua kumuozesha binti yake baada ya binti huyo
kumtaarifu kuwa amepata mchumba.
Kwa upande wa binti huyo amesema kuwa alikutana na kijana huyo Juma
(20) na kumwambia kuwa anampenda lakini yeye aliona kuwa anamtania na
kuamua kuachana naye.
Hata hivyo baadhi ya majirani wa mama huyo wamesema kuwa ni tabia ya
mama huyo ambaye ni mjane kuwaozesha watoto wake wakiwa katika umri
mdogo kwani kuna mwanaye mmoja mwenye umri wa miaka 14 alibebeshwa mimba
na mpaka sasa ana mtoto mdogo anayemlea.
Naye mwenyekiti wa mtaa huo, Nashoni Chinywa amesema kuwa baada ya
mahojiano mama huyo alikiri kosa lake na kusema kuwa amechochwa na
malezi ya watoto hao kwani hata dada yake mwenye umri wa miaka 14
alibebeshwa mimba akiwa nyumbani hivyo akaona ni bora amuozeshe na huyo
mdogo wake ili asije akabeba mimba nyumbani
No comments:
Post a Comment