
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara (wapili kulia)
akitoa maekekezo kwa Viongozi wa TTCL katika ziara yake Mkoani Mtwara
juzi.

Wafanyakazi wa TTCL Mtwara katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi
ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette na Ofisa Mtendaji Mkuu wao, Dk. Kamugisha
Kazaura.

Ofisa Mtendaji Mkuu wao, Dk. Kamugisha Kazaura (wa kwanza kushoto)
akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Prof Makame Mbawara mkoani Mtwara juzi.

Mazungumzo kati ya Wafanyakazi wa TTCL Mtwara katika mkutano na Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara alipofanya ziara
yake.
SERIKALI
ipo katika hatua za mwisho za kuilipa kampuni ya Bharti Airtel ili
kurejesha umiliki wa asilimia 100 katika Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL.
Uamuzi huo unaotarajiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwezi huu
utaiwezesha TTCL kurejesha hisa zake 35% zilizonunuliwa na Airel mwaka
2001 na kuifanya Bharti Airtel kuwa mbia mwenza katika Kampuni hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa ametangaza
uamuzi huo Jumatatu hii Mkoani Mtwara alipotembelea Ofisi za TTCL Mkoa
wa Mtwara, kukagua mitambo na miundo mbinu ya Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano.
"Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha Watanzania na wadau wote wa
TTCL kuhusu kuondoka kwa mbia mwenza Kampuni ya Bharti Airtel. Ubia huu
wa TTCL na Bharti Airtel utahitimishwa Rasmi kabla ya mwisho wa mwezi
huu.
Tumefanya majadiliano ya kutosha, tumekubaliana kuwa Serikali iilipe
Bharti Airtel sh bilioni 14.9 ili kurejesha hisa za 35% za TTCL na
kuifanya Kampuni hii ya TTCL kuwa mali ya Umma kwa 100%.
Tutatumia fedha za Mapato ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili
kukamilisha utaratibu huu. Naiagiza Bodi na Menejimenti ya TTCL kufanya
kazi kwa bidii na Ufanisi Mkubwa na kusimamia kikamilifu shughuki za
TTCL ili kutimiza jukumu lake kwa Umma. Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Bodi ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette amesema, kukamilika kwa mchakato huu
ni hatua muhimu sana kwa Uhai na ufanisi wa TTCL na kusisitiza kuwa,
mpango wa mageuzi ya kibiashara wa kampuni hiyo sasa utatekelezeka kwa
kasi kubwa baada ya hatua hii.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura amesema, jitihada
kubwa za TTCL sasa zitaelekezwa katika kuboresha huduma kwa kutumia
fedha za ndani na Mikopo ya wadau wa kibiashara ili kuiwezesha kampuni
kuendelea kuwa kiongozi katika utoaji wa huduma bora na nafuu katika
soko la Mawasiliano nchini.
Hivi karibuni, TTCL imezindua huduma za Mtandao wenye kasi zaidi wa 4G
LTE na kuimarisha ubora wa huduma zake za data na sauti.
Aidha, TTCL na Benki ya TIB zimeingia makubaliano ya mkopo wa fedha na
dhamana za Benki utakaoiwezesha TTCL kupata fedha dola za Marekali
milioni 329 ili kuingiza mitambo mipya ya kisasa itakayo boresha huduma
zake ikiwa ni pamoja na kuanzisha huduma ya miamala ya fedha kwa njia ya
mtandao.
No comments:
Post a Comment