
Mcheza filamu raia wa kenya Lupita Nyong’o ameungana na wacheza
filamu wengine kushutumu kutojumuishwa kwa wacheza filamu weusi au wale
wachache kutoka kwa orodha ya wale wanaowania tuzo za Oscars.
Katika akaunti yake ya Istagram Lupita amesema amekasirishwa sana na kukosa kujumuishwa kwa wacheza filamu weusi.
Mwaka 2014 Lupita Nyong’o alishinda tuzo la Oscar kutokana na wajibu wake katika filamu ya Twelve Years a Slave.
Mwaka 2014 Lupita Nyong’o alishinda tuzo la Oscar kutokana na wajibu wake katika filamu ya Twelve Years a Slave.
Anaungana na wacheza filamu wanaozidi kuongezeka wakiwemo David
Oyelowo na Don Cheadle ambao wamekosoa tuzo za Oscars kuwa kukosa kuteua
watu kutoka tabaka zote.

Wiki iliyopita Jada Pinket mkewe nyota wa filamu Will Smith amesema
hatashiriki katika tuzo za Oscar, Nyota huyo aliandika katika mtandao
wake wa Tweeter mwishoni mwa wiki akionyesha kukasirishwa na ukosefu wa
watu wa rangi tofauti miongoni mwa wale walioteuliwa kuwania tuzo za
Oscar.
Katika msururu wa ujumbe huo katika mtandao wa Twitter,Jada mwenye
umri wa miaka 44 alishangazwa alipogundua kwamba hakuna nyota weusi
walioteuliwa katika orodha za juu wakati uteuzi huo ulipofanywa.

No comments:
Post a Comment