TTCL

EQUITY

Tuesday, January 12, 2016

TALGWU walaani viongozi wanaotumia madaraka vibaya

Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa nchini Tanzania TALGWU kimelaani vitendo wanavyofanyiwa wafanyakazi wa serikali za mitaa na baadhi ya viongozi wa wilaya nchini na kutumia vibaya kauli mbiu ya hapa kazi tu.
Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa nchini Tanzania TALGWU kimelaani vitendo wanavyofanyiwa wafanyakazi wa serikali za mitaa na baadhi ya viongozi wa wilaya nchini na kutumia vibaya kauli mbiu ya hapa kazi tu kwa kuwanyanyasa wafanyakazi hao ikiwa ni tabia iliyozuka hivi karibuni.

Akitolea mifano ya baadhi ya viongozi wanaotumia kauli ya hapa kazi tu kaimu katibu mkuu wa TALGWU Kibwana Njaa ametaja baadhi ya viongozi nchini kuwa wamekuwa wakiwanyanyasa wafanyakazi huku wakikosa ukweli wa makosa na kutumia vyombo vya habari ili kuwahukumu waonekane wakifanya kazi.

Njaa amesema kuwa TALGWU inaendelea kuunga mkono kauli mbiu ya Hapa kazi tu lakini inakemea matumizi mabaya ya kauli mbiu hiyo inayotumiwa hivi sasa na baadhi ya viongozi hao kunyanyasa wafanyakazi wa serikali za mitaa nchini..

No comments:

Post a Comment