TTCL

EQUITY

Tuesday, January 12, 2016

Msifanye ardhi kama biashara: Lukuvi

 
Serikali inatarajia kutoa bei elekezi ya uuzaji wa ardhi, tofauti na hali ya sasa ambayo viwanja vimekuwa vikiuzwa kwa bei ya juu na kufanya watu wasio na uwezo kiuchumi kushindwa kumiliki na kujenga nyumba.


Hayo yamesemwa na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi, alipokuwa akizungumza na watendaji na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Lukuvi amebainisha kuwa kwa maeneo ambayo eneo la ardhi ni kubwa litapimwa na kuuzwa kwa bei elekezi itakayotangazwa na serikali ili kuondoa ubabaishaji na kufanya kazi hiyo iwe rahisi kuliko ilivyo hivi sasa.



''Kuna maafisa ardhi wamefanya ardhi kuwa kitega uchumi chao hawapimi ardhi kwa wakati ili kuondoa hali hii lazima tutoe bei elekezi kwa eneo lililo kubwa''
Amesema bei dira hiyo itakuwa kwa watu wote wanaouza ardhi kwa maana kwamba, kabla ya kuuza, watatakiwa kuwasiliana na serikali ili wananchi wapunguziwe kero ya kushindwa kumiliki ardhi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo. Alisema ardhi ni huduma na si biashara.

Hata hivyo waziri Lukuvi amesema baadhi ya watu wamefanya ardhi, kama ndiyo sehemu ya kujinufaisha kwa kununua mashamba, kisha kuyagawa viwanja ambavyo huviuza kwa bei kubwa.
Amesema jambo hilo limekuwa likisababisha wananchi wa kawaida, kushindwa kumudu kununua viwanja.

No comments:

Post a Comment