Rais
wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein
amesema mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar yanaendelea na
hayajasita ingawa amesisitiza kuwa marudio ya uchaguzi mkuu zanzibar
upo na utarudiwa.
Dr Shein ambaye mara baada ya kuwasili uwanjani alikagua Gwaride la
heshima liliondaliwa na vikosi vya ulinzi na uslama vya jamhuri ya
muungano wakiwemo JWTZ na polisi na vikosi vya SMZ ambapo akitoa msimamo
huo wa serikali katika hotuba yake kwa wananchi wa Zanzibar katika siku
ya kilele cha sherehe za miaka 52 ya mapinduiz ya Zanzibar
zilizofanyika uwnaja wa Amani na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi
wakiwemo viongozi wa serikali zote mbili wakiongozwa na rais John
Magufuli, waziri mkuu kassim Majaliwa, makamu wa rais Samia Suluhu,
marais wastaafu wa muungnao Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa na Jakaya
Kiwete pamoja na rais mstaafu wa Zanzibar Dr Amani Abeid Karume na
viongozi waandamizi wa serikali zote mbili.
Rais wa Zanzibar katika hotuba yake hiyo kwa wananchi alizumgumzia
suala la amani na utulivu wananchi na kuahidi kuhakiksha suala la amani
inalindwa wakati wote huku pia akisisitiza kuwa muungano wa Tanznaia
utalindwa kwa nguvu zote kwa vile upo kikatiba na sheria ambapo pia
alizungumzia suala la uchumi wa Zanzibar.
Mapema makamu wa pili wa rais Balozi Seif Ali Iddi amesema
mapinduzi ya 1964 ni kigezo cha wazanzibari kuwa huru katika nchi yao na
ishara ya wazanzibari kuondoa utawala uliokuwa ukiwakandamiza wananchi
hivyo daima yatalindwa.
Mapema Dr Shein alipokea maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya
Zanzibar na pia wafanyakazi wa wizara na taasisi za serikali ya Zanzibar
na muungano na pia kushuhudia kikosi cha makomandoo wa JWTZ wakipita
kikakamavu na kivita ambao walipita mbele ya jukwaa kuu na pia
kushuhudia Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vilivyopita kwa
mwendo wa kasi na pole.
No comments:
Post a Comment