TTCL

EQUITY

Monday, January 25, 2016

Serikali yamsimamisha kazi msimamizi wa Bomoabomoa

Makosa yaliyoainishwa na Waziri Makamba ni pamoja na ukiukwaji mkubwa wa miiko ya kazi katika kushughulikia kiwanda kilichokuwa kikichinja punda Mkoani Dodoma,pili usimamizi wao wa kazi sio makini na dhabiti jambo ambalo linasababisha malalamiko kwa wananchi.
Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Dkt. Eladius Makene ambaye alikuwa afisa mwandamizi wa mazingira pamoja na Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi afisa mazingira ambapo hatua nyingine za kinidhamu zitachukuliwa dhiidi yao.
Aidha waziri amesema ataunda jopo la wataalamu wa kuichunguza NEMC namna ambavyo inashughulikia mazingira hapa nchini ili tume hiyo itoe ushauri kwa serikali.
Hata hivyo waziri ameitaka NEMC kuitisha mkutano wa dharura ndani ya wiki tatu ilikujadili changamoto za utendaji wa baraza hilo.

No comments:

Post a Comment