TTCL

EQUITY

Tuesday, January 12, 2016

Serikali yasema haitovumilia maeneo yake ya hifadhi za taifa kuendelea kuhalibiwa na wananchi.

Serikali imesema kuwa haito vumilia kuona maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi hususani hifadhi za taifa yanaendelea kuhalibiwa na baadhi ya wananchi wanaofanya uhalifu kwa makusudi ndani ya hifadhi ikiwemo kuendesha shughuli za ufugaji, kilimo, makazi na ujangili kwa kigezo cha kutolewa kwa adhabu ndogo kwa washitakiwa wa makosa hayo pindi wanapokamatwa jambo ambalo linasababisha kuongezeka na kurudiwa mara kwa mara kwa makosa hayo.

Akizungumza katika ziara yake aliyoifanya katika hifadhi ya taifa ya Serengeti na kushuhudia idadi kubwa ya mifugo, mazao na baadhi ya wananchi wakidiliki kujenga ndani ya alama za mwisho wa hifadhi hiyo huku wakijua kufanya hivyo ni kosa naibu waziri wa maliasili na utalii Mhe Mhandisi Ramo Makani amemwagiza mkurugenzi mkuu wa hifadhi za taifa-TANAPA kuwakilisha mara moja rasimu mpya ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria kwa kuboresha kipengele cha adhabu ili ziendane na thamani ya uharibifu unao fanyika.
 
Wakati huohuo Mhe Ramo amezungumzia mikakati ya serikali ya awamu ya 5 ya kupambana na ujangili hususani wa Tembo.
 
Katika taarifa yake mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Serengeti-TANAPA ameitaja changamoto kubwa inayoikabili hifadhi hiyo yenye adhi ya kimataifa ni ujangili ambao umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika kipindi cha mwaka 2014-2015 wahalifu zaidi ya elfu 1 na jumla ya bunduki 109 zikiwemo slaa nzito aina ya SMG zikikamatwa.

No comments:

Post a Comment