TTCL

EQUITY

Friday, January 15, 2016

Mwana FA na Swaga za Asanteni kwa Kuja

mwana Fa 
Mwana FA
Tayari msemo wa asanteni kwa kuja ambao ni jina la ngoma mpya ya Mwana FA aliyoiachia hivi karibuni  meeleweka mitaani, unatumiwa na watu wengi kwa sasa, katika mitandao ya kijamii ndiyo usiseme.
Ni swaga f’lani mtu akitaka kutupa dongo kwa ‘masnitch’ wake au kujibu mashambulizi akamalizia na msemo huo ‘asanteni kwa kuja.’
Ukweli ni kwamba kwa sasa msemo huo ndiyo habari ya mjini, lakini mbali na kupaa kwake kitaani bado mashabiki wengi wa muziki wamekuwa na maswali mengi juu ya maana halisi ya wimbo huo.
Showbiz ilipiga stori na FA kufafanua baadhi ya vesi.
Ijumaa: Hongera kwa video kali ya Asanteni Kwa Kuja uliyoiachia Jumatatu iliyopita, unaweza kuwaambia wasomaji kuanzia audio mpaka video umefanyia wapi?
FA: Audio niligongea kwa Hermy B, B-Heat Records lakini kichupa nilifanya Sauzi kwa Spice Pictures.
Ijumaa: Asanteni Kwa Kuja imekuwa swaga mpya kitaani, lakini kutokana na mashairi yake, wimbo unaonekana ni dongo kwa msanii ambaye ni jamaa yako, funguka!
FA: Sijamlenga mtu yeyote hiyo ni idea tu, lakini kama yupo anayehisi unamhusu poa tu ni sawa na kurusha jiwe gizani.
Ijumaa: Sawa, hebu tucheki baadhi ya mashairi, umeanza kwa kutaja neno ‘kwaya masta’ ulikuwa unamaanisha nini? Au unamlenga nani?
FA: Hahaa! Hakuna, nilikuwa namaanisha mimi mwenyewe na uwezo wangu wa kuimbisha watu nikiwa
stejini.
Ijumaa: Kwenye verse ya kwanza kuna mistari inasema;…sio salama sio salmini na silali ka vitani… hakuna imani kwa masnitch mwana…njoo na panga ukute shoka ka’ zamani zama…bastola na glasi ya vodka, lazima kuwa na  adaka…madeni lazima yalipwe hata mdaiwa
asipotaka’. Hapa inadaiwa umemtis GK, kuna ukweli?
FA: No, mimi na GK hatuna tofauti, yule ni kama broo wangu, lakini niseme tu wazi asili ya Muziki wa Hip Hop ni ‘bato’ na sasa naona kama watu wamelala na hakuna ushindani.
Ijumaa: Vipi kuhusu mistari hii, dizaini kama kuna mtu unamwambia; ‘wenye kelele wote sio Kings, kuwa na nidhamu… tatizo la uongo ni kwamba milele haufiki mwisho…kaa kiporo utatudanganya na kesho…malalamiko kibao ka’ mtoto wa kambo… kurukaruka haijawahi kuwa dawa ya ulimbo…
FA: Ni kweli, mistari inajieleza, niwasihi tu watu wasipende kuamini kila wanachokisikia na kuwachukulia poa watu wanaoweza kuwarudisha nyuma kwenye harakati zao, ili kuwaonesha kuwa unaweza fanya kweli.
Ijumaa: Tumalize na verse ya mwisho kwenye hii mistari; ‘hata mi ni hater ka’ hunipendi hivyo hivyo bro…ulete ubwege na nikupende mi ni Yesu?… hakuna shavu la pili toa wembe nitoe kisu… bado mshabiki mkubwa wa kazi ya Mungu… ila kama nakuweza simngoji nakupa kubwa wangu…life yangu movie na mi ndio director… hata ukinielekeza sio kitu unakuwa extra…
FA: Hapo niliongelea udhaifu ninaoweza kuwa nao kama mwanadamu, mtu akizingua pia nazingua, kikubwa najiamini, maisha yangu nayaendesha mwenyewe, siwezi kufeli kisa mtu fulani niliyekuwa naye hayupo.

No comments:

Post a Comment