Baadhi ya viongozi wa siasa nchini wametaka wigo
wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar upanuliwe kwa
kushirikisha wadau wote badala ya kuviachia vyama vinavyovutana vya CCM
na CUF peke yao.
James Mbatia ni mmoja wa Viongozi wa Umoja wa UKAWA, na Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa chama cha
NCCR-Mageuzi, Mhe. James Mbatia jana ametoa maoni juu ya mgogoro wa Zanzibar ambapo ametaka mgogoro huo kutatuliwa kwa
mujibu wa Katiba ya Zanzibar pamoja na kuhusisha kituo cha demokrasia
nchini ili kupata suluhusu ya suala hilo.
Mhe. Mbatia amesema kuwa mgogoro huo wa kikatiba usipotatuliwa na
kufuata busara ya kuwahusisha wadau tofauti unaweza kusababisha
machafuko visiwani humo na kuliharibia jina taifa pamoja na kugharimu
maisha ya watanzania.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha Sauti ya Umma (SAU),
Bw. Yusuph Manyanga amesema kuwa majadiliano ya vyama viwili kwa sasa
hayalengi kutafuta suluhisho kutokana na kila chama kuvutia upande wake.
No comments:
Post a Comment