TTCL

EQUITY

Wednesday, January 13, 2016

CCM yaomba radhi watanzania

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi, ulioandikwa kwenye moja ya mabango yaliyobebwa na mmoja wa wananchi, waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa mawasiliano na umma wa CCM, Daniel Chongolo, jijini Dar es Salaam imesema Chama cha Mapinduzi kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.

“Ujumbe huo, sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi, bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na shabaha ya waasisi wa mapinduzi hayo matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza umoja na mshikamano wa kitaifa,” ilisema taarifa hiyo.

Katika maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar yalipambwa na maandamano ya wafanyakazi na wanafunzi ambapo bango moja lilisomeka ''Machotara hizbu Zanzibar ni nchi ya waafika'' bango ambalo limezua utata nchini.

No comments:

Post a Comment