TTCL

EQUITY

Tuesday, January 12, 2016

Wilfred Kidau atoa somo kwa makocha wazawa

Makocha wazawa nchini wametakiwa kuzingatia weledi wa kazi yao kwa umakini mkubwa ili kuongeza ushindani kwa makocha wa kigeni wanaoonekana kuwa ndio bora zaidi yao kwenye klabu mbalimbali hapa nchini.

Mkufunzi wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF katika picha .
Akizungumza na East Africa Radio mkufunzi wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Wilfred Kidau amesema haoni utofauti wa makocha wazawa na wale wa kigeni ambao wanaonekana kupewa kipaumbele na viongozi wa klabu nyingi hapa Tanzania.

Kidau ameongeza kuwa tatizo kubwa ni makocha wengi wazawa wanakosa mafunzo mengi ya vitendo ambayo yangewasaidia kujua kile wanachojifunza kwa nadharia darasani na namna ya kukifundisha viwanjani.

Aidha mkufunzi huyo amewataka makocha kujitahidi kwa hali na mali kujiamini na kuonesha wana uwezo kama ilivyo kwa Mecky Mexime ambaye anaonesha ubora wake na klabu ya Mtibwa Sugar inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Pia Kocha wa siku nyingi na mchambuzi wa mpira wa soka nchini Tanzania Kenny Mwaisabula "Mzazi" amesema klabu ya Simba haipo makini katika kuchagua makocha sahihi na ndio maana inatimua makocha kila wakati.
Kocha wa siku nyingi na mchambuzi wa soka nchini Tanzania Kenny Mwaisabula "Mzazi" amesema klabu ya Simba haipo makini katika kuchagua makocha sahihi na ndiyo maana inatimua makocha kila wakati.

Mwaisabula amesema ni kitu cha kushangaza kwa Simba kumfuta kazi Dylan Kerr wakati hadi sasa ameifikisha Simba nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Mwaisabula ambaye aliwahi kuifundisha klabu ya soka ya Yanga, amesema Simba kuna tatizo la maamuzi ya kutafuta makocha, hivyo baadhi yao wanageukana pale mambo yanapoharibika na akaitaka ikae chini na kufikiria wapi wanakosea.

Uongozi wa Simba umeachana na kocha huyo baada ya miezi 6 ya mkataba wa mwaka mmoja na kuvunja huko mkataba ni makubaliano ya pande mbili.

No comments:

Post a Comment