TTCL

EQUITY

Thursday, December 24, 2015

Wakurugenzi wanaoingia mikataba mibovu waonywa

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina amekemea Wakurugenzi wa Manispaa wanaoingia mikataba mibovu.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina amekemea Wakurugenzi wa Manispaa wanaoingia mikataba mibovu na wawekezaji wasioweza kufanyakazi kwa wakati muafaka na kwa uhakika na kuacha kuingia mikataba ya kifisadi.

Mhe. Mpina ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika mahojiano na East Africa Radio amesema tayari ofisi yake imeshaagiza wakurugenzi wote nchini kupitia tena mikataba ya magari ya kuzoa taka na kutoa ripoti kwa serikali ili kuangalia upya taratibu za mikataba zitakazoendana na kodi ya wananchi wanayoitoa.

Aidha, katika hatua nyingine Mhe. Mpina amewataka wamiliki wa magari ya kuzoa takataka kubadilisha mfumo wa uzoaji taka na waanze kufanya shughuli hiyo mida ya usiku na wahakikishe magari yao wanayafunika kuzuia kudondosha ovyo taka kwenye makazi ya watu.

No comments:

Post a Comment