Kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL) imezindua rasmi teknolojia ya Long Term Evolution
(LTE) inayojulikana kwa jina la mtandao wa 4G. Awamu ya kwanza inayoanza
leo siku ya uzinduzi itatoa huduma katika maeneo 11 Jijini Dar es
salaam.
Maeneo hayo
ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Mwl J.K. Nyerere, Pugu Road, Posta
Mpya, Upanga, Kinondoni, Ubungo, Oysterbay, Mwenge, Mbezi Tangibovu,
Mbezi Exchange, Kunduchi Salasala na Wazo Tegeta. Awamu pili itakuwa
kupeleka mawasiliano hayo katika maeneo mengine ya Jiji la Dar Es Salaam
na kasha kusambaa kote nchini.
Huduma hii
itaambatana na vifurushi ambavyo vya intaneti vilivyoboreshwa zaidi
kulingana maisha ya mtanzania. Mafanikio haya ya kuboresha teknolojia na
vifurushi vya intaneti vitarahisisha mawasiliano miongoni mwa wananchi
na kukuza matumizi ya TEHAMA nchini. Aidha, kuanza kwa huduma za 4G LTE
ya TTCL kutakamilisha nia ya siku nyingi ya Kampuni ya kuwahudumia
kikamilifu wateja katika nyanja zote za mawasiliano(Fixed& mobile
convergence).
Faida za Mtandao wa 4G LTE
Mtandao huu
wa 4G-LTE utakuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuongeza kasi ya
shughuli za maendeleo kijamii na kiuchumi, kuchangia katika kukuza
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuongeza uzalishaji katika sekta
mbalimbali za maendeleo.
TTCL
tunaamini kuwa Mtandao wa 4G- TTCL utafungua fursa pekee katika kukuza
sekta ya elimu nchini kwa njia ya mtandao( E education). Ubora wa
intaneti hii itatoa fursa kwa wanafunzi, walimu, wakufunzi, wataalamu na
wanazuoni kutumia teknolojia katika kujifunza mambo mbalimbali ya
kitaaluma na nje ya taaluma.
Mtandao wa
4G LTE utaongeza fursa katika sekta ya Afya ambapo hospitali, vituo vya
afya, vyuo vya afya na wadau mbalimbali wataweza kutumia mtandao huu
katika kuongeza ufanisi wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa
haraka na uhakika zaidi. Kiwango cha spidi ya intaneti ya 4G kina uwezo
wa kufanikisha kikamilifu programu za kutoa huduma za afya kwa mtandao
(Telemedicine).
Aidha,
mtandao huu pia utanufaisha sekta nyingine za kiuchumi kama vile sekta
ya Biashara. Wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa wanahitaji
mawasiliano ya ukakika katika shughuli zao. Mtandao huu wa 4G-LTE
utakuwa mkombozi wao, na utaleta mageuzi katika kuongeza uzalishaji,
kupanua wigo wa masoko ya bidhaa kwa wakulima, masoko kwa
wajasirilimali, masoko kwa makampuni ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania.
Pamoja Tunaweza, TTCL- huleta watu Karibu.
No comments:
Post a Comment