TTCL

EQUITY

Tuesday, December 22, 2015

KLICK MY POINT;

Duh mwaka umeishaaa hope kwenye list ya vitu vyako uloandika kwa mwaka huu kufanikisha at least umefanya robo au nusu yake.
Karibu kwenye Kipengele kipya kabisa cha Klick my point, hapa ni pahala ninapokuletea matukio muhim na adhim kabisa, utapata kuona na kuwafaham watu wanaofanya mambo muhimu na yanayolenga jamii kwa undani, kwa leo nakupa habari mchanganyiko ni kiwahusisha watu mbalimbali waliohusika kutoa fursa, ama kuifikia jamii kwa namna fulani.

zama
Hongera sana Zamaradi umefanya kitu kizuri, kitu kipya, kids festival yaonyesha watoto wali enjoy na kujiona na wao wanayo fursa katika jamii. huu uwe mwanzo mzuri, zije nyingine nyingi na nzuri zaidi kwa sababu watoto ni moja ya jamii zilizo sahauliwa katika ulimwengu wa sanaa ya ubunifu n.k
matata
Flaviana Matata in shades of  Gery and black love the look soo classy.
Flaviana Matata ni jina la Mtanzania ambalo kila siku zinavyosogea linazidi kutajwa zaidi kwenye orodha ya Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi, wanaliwakilisha vizuri taifa la Tanzania na hata kukumbuka pia nyumbani.
Headlines zake kubwa zilizofanya wengi wawe upande wake pia ni ishu aliyoibuni kupitia Flaviana Matata Foundation kuwasaidia Watoto wa kike shuleni.
Kingine kipya kwa sasa ni Flaviana matata kuendelea kupata mafanikio kwenye kazi ya mikono yake baada ya kupata dili la kutangaza vipodozi vya Kiko Milano vya Italy kwenye kampeni ya Modern Tribe kwa mujibu wa >> 8020Fashionblog

846067217

Mohammed Dewji ‘MO’ alipohitimu masomo mwaka 1998 alirudi nyumbani Tanzania na moja kwa moja akaingia kwenye biashara za baba yake Mzee Gulam na akaanza na nafasi ya Mdhibiti mkuu wa Fedha katika kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL).
Mbali na kuingia kwenye biashara, Mo alijiingiza kwenye michezo na kuanza kuifadhili Simba Sports Club ya Dar es Salaam. Huu ukawa mwanzo wa Watanzania kumuona Mo akiingia kwenye ulimwengu wa michezo wa Tanzania na hasa soka.
Ilipofika mwaka 2000, uchaguzi wa pili wa mfumo wa vyama vingi nchini uliwadia. Na Mo akajiingiza kwenye kinyanganyiro hicho akiwania kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Singida mjini. Katika kura za maoni Mo alimshinda Waziri wa Maji wa wakati huo Musa Nkhangaa kwa kura nyingi lakini kamati kuu ya CCM hawakumpitisha kugombea ubunge.
Kuna usemi mvumilivu hula mbivu, hivyo Mo akakubali na kuheshimu maamuzi ya chama na kumpigia kampeni mgombea wa chama na kuhakikisha wanashinda Uchaguzi wa 2000.
Pamoja na kushindwa kupata nafasi ya kugombea ubunge, Mo aliwasaidia wananchi wa Singida kwa hali na mali , huku pia akizidi kutoa mikataba minono ya udhamini kwa Simba iliyokuwa inazidi Milioni mia moja kwa mwaka.
Chini ya uongozi wake kampuni imepanda ngazi nyingi za mafanikio na kukua mara nane ya kiwango alichokikuta kuanzia pale alipoanza kufanya kazi, amewekeza kwenye sekta tofauti kama Kilimo, Fedha, Uzalishaji na Usambazaji wa bidhaa. Takwimu zinaonyesha kampuni za Mo zinachangia pato la ndani la taifa kwa asilimia mbili na zinaajiri zaidi ya watu 20,000.
Mwaka 2005 ulikuwa mwaka wa uchaguzi na MO akachukua fomu tena za kuwania ubunge wa jimbo la Singida mjini. Kwa mara nyingine aliibuka kidedea katika kura za maoni akipitishwa na kamati kuu ya CCM kuwa mgombea na baada ya hapo akawabwaga wapinzani wake katika uchaguzi kwa kuchaguliwa kwa zaidi ya asilimia tisini ya kura zote zilizopigwa.
Ili kufanikisha na kuleta maendeleo ya Stars kamati maalumu ya ushindi iliundwa huku Mo akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wake. Katika kipindi chake Taifa Stars wamebadilika kutoka kuwa kichwa cha mwendawazimu na kuwa timu inayoheshimika barani Afrika ikitoa sare na vigogo wa soka kama Cameroon na Senegal .
Pia chini ya uenyekiti wake Taifa Stars imepata kushiriki michuano mikubwa barani Afrika ya CHAN yaliyofanyika nchini Ivory Coast.

kwenye listi wapo wengi lakini leo nakupa hao wachache na kabla hatujaumaliza mwaka nitakupa tena fursa ya kuwatambua wengine na mambo makubwa waliyoshiriki kijamii n.k hii yote ni kukuonesha kuwa inawezekana, piga hatua usikate tamaa, mawazo uliyonayo kuhusu maendeleo ni ya thamanii kubwa haijalishi ni maendeleo yako binafsi au kwa jamii. usikose Click my point, inakujia tena hapa hapa....

No comments:

Post a Comment